Mshambuliaji wa zamani wa vilabu vya Tukuyu Stars na Prisons
vya Mbeya John Joseph amekamatwa na jeshi la polisi mkoani Mbeya akiuza tiketi
bandia kwenye mchezo wa Mbeya City na Mtibwa Sugar.
John Joseph ambaye kwasasa ni askari wa jeshi la Magereza mkoani
humo,alikamatwa na tiketi tano bandia akiziuza nje ya uwanja wa Sokoine.
Akiongea hapo jana usiku kwenye kipindi cha SPORTS BAR cha Clouds TV
kinachoruka kila ya Jumatatu, kamanda wa polisi wa mkoa wa Mbeya ndugu Ahmed Msangi
alithibitisha kukamatwa kwa askali huyo na kusema uchunguzi ukikamilika
atapelekwa mahakamani.
Hapa John Joseph akiwa ameshikiliwa na polisi.
Tiketi halali.....imeiva....
Hii ilikuwa tiketi feki......imepauka
0 comments :
Post a Comment