MABAO
mawili toka kwa Mwanasoka Bora wa zamani wa dunia, Kaka na jingine na
'mtukutu' Mario Balotellu yalitosha kuipa ushindi mnono AC MIlan kwenye
uwanja wake wa nyumbani kwa kuifumua Chievo Verona mabao 3-0 katika
mfululizo wa Ligi Kuu ya Italia.
Ushindi huo wa
pili mfululizo umeifanya Milan kuchupa kutoa nafasi ya 12 hadi ya 9 na
kufufua matuamini ya kocha wake Clarence Seedorf.
Balotelli alianza kufunga bao la mapmea
dakika ya nne tu ya mchezo huo kumalizia kadi ya Rami kabla ya Kaka
kuongeza la pili dakika ya 27 na kuipeleka Milan mapumziko wakiwa mbele
kwa 2-0.
Kipindi cha pili Kaka aliongeza jingine katika dakika ya 54 na kuifanya Milan kufikisha jumla ya pointi 42.
Katika mechi nyingine ya ligi iliyochezwa jana Atalanta ikiwa ugenini iliichapa Bologna kwa mabao 2-0.
0 comments :
Post a Comment