Mwanamke aliyetajwa kwa jina la Jessica Dutro, anakabiriwa na kesi ya mauaji huko Washington Marekani baada ya kutuhumiwa kuwa alimpiga mwanae wa miaka 4 hadi kumuua baada ya kuhisi kuwa atakuwa ‘shoga’.
Waendesha
mashitaka walidai kuwa August 14, 2012 mama huyo aliwapiga vibaya
watoto wake watatu, lakini kipigo kilikuwa kikali zaidi kwa mwanae
aitwae Zachary Dutro- Boggess ambaye alimuudhi zaidi baada kuona kuwa
anatabia za kishoga mapema akiwa mtoto.Baada
ya kipigo kikali mtoto huyo alipelekwa hospitalini siku hiyo na kitengo
cha dharura na kuwekwa kwenye mashine ya kumsaidia kupumua, hata hivyo
baada ya siku mbili alipoteza maisha
0 comments :
Post a Comment