.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

ALICHOKISEMA CASILLAS KUHUSU TETESI ZA KUHAMIA ARSENAL

Hispania- Real Madrid
Golikipa wa Real Madrid Ike Casillas, ambae mpaka sasa amecheza mechi zaidi ya 600 akiwa na madrid tangu ajiunge mnamo mwaka 1999, amesisitiza kwamba hayupo tayari kuondoka katika klabu hio na amepanga kustaafu mpira akiwa na timu hio inayoshiriki ligi kuu ya Hispania

Ike Casillas (32) amekua akikaa benchi tangu msimu uliopita walipokua na kocha wao wazamani Jose Mourinho alie amua kumuanzisha Diego Lopez. Hata baada ya Carol Ancelloti kuchukua nafasi ya Mourinho, Casillas ajaona mabadiliko yeyote yale.

casillas yuko katika mkataba na Real Madrid mpaka Juni 2017 ila habari ya siri inasema yupo katika hatua za kujiunga na Arsenal katika usajili wa Majira ya Joto.  Ila mchezaji huyo alifunguka na kusema kwamba yeye yupo katika msimamo wake wa kucheza madrid mpaka mkataba wake utakapo kwisha.

"nafikiria sana na sana kuhusu ntakachofanya mara tu ntakapo staafu kucheza mpira. Ningependa kuendelea kujihusisha na mpira na kusaidia klabu yangu, kama hali ikiruhusu," alisema Casillas


"Naweza kucheza mpaka ntakapokua na miaka 40. kama unapenda kuwa Goli kipa, basi unaweza kucheza mpaka umri huo" 

"Ningependa kuendelea kucheza Real madrid mpaka nifike miaka 40, ila itafika mdaa ambao itakua aiwezekani tena kucheza. Nitajua kuhusu maisha yangu ya baadae na Madrid pindi mkataba wangu utakapo malizika." aliongezea Casillas

"Ningependa kuendelea kushinda makombe." alisema Casillas
Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad