Imeshawahi kuandikwa baada ya stori kusambaa kwamba mwimbaji mtanzania Diamond Platnumz ana uhusiano wa kimapenzi na mwimbaji Mkenya Victoria Kimani ambae ni dada wa rapper Bamboo, rapper huyu alisema Diamond hana hadhi ya kutembea na mdogo wake.
Inawezekana hii kauli ya staa huyu wa ‘compe’ labda iliwafanya baadhi ya watu waone kama hampendi Diamond ila kiukweli, staa huyu ambae ni msanii anaependa kujihusisha na muziki unaoinua watu kimaisha pia, amekua mkweli kuhusu jitihada zinazofanywa na Diamond kwenye muziki.
Kwenye Exclusive interview na millardayo.com pamoja na AyoTV Nairobi Kenya, Bamboo amesema ‘kitu kizuri au kikubwa ninachokiona kwenye muziki wa bongofleva sasa hivi ni kile kinachoonekana kwenye Channel O, MTV au East Africa TV na ninachokiona ni kwamba Diamond anang’aa sana sehemu hizo’
‘Sio kwamba mimi ni shabiki wa Diamond lakini kiukweli Dimond ni msanii ambae anafanya kazi kwa bidii na kuelewa ni kitu gani anatakiwa kukiwasilisha, napenda kuona msanii mwenye bidii kama yeye kwenye kazi… anajua anachofanya’ -Bamboo
0 comments :
Post a Comment