Ikiwa imebaki miezi miwili kabla ya kuanza kwa mashindano ya Kombe la Dunia ambayo safari hii yatafanyika nchini Brazil.
Wananchi wa Brazil ambao siku kadhaa zilizopita wameonekana wakiandamana kupinga Kombe la Dunia kufanyika nchini kwao kwani inagharimu pesa nyingi ambazo wanaweza kupewa wananchi ili kuongeza hali yao ya maisha na elimu kiujumla.
Vikosi vya Wanajeshi wameonekana wakiwa wametanda katika mji wa Complexo da Mare ambao mji huo upo karibu na Kiwanja cha ndege kikuu cha Rio, Complexo de Mare miji inayoongoza kwa uhalifu na uhuni nchini brazil,
Huku ikitegemewa wageni wote kutumia kiwanja kikuu cha Rio na pia kupita katikati ya mji wa Complexo da Mare wakiwa wanaelekea Mjini kwenye makazi walioandaliwa. Hofu imetanda sana kuhofia wageni kuvamiwa au kutekwa wakiwa wanaelekea mijini kwenye makazi.
Vikosi vya wanajeshi wametanda mitaa ya Complexo da Mare wakiwa na vifaru na helikopta wakiwa na dhumuni la kuwasaka majambazi na wahuni waliojificha katika mitaa hio.
Viongozi wa Brazil wanakanusha, kwamba kuondoa majambazi hao haiusiani na Kombe la Dunia ila ni kwa ajili ya kulinda maisha ya Rio na Mare.
0 comments :
Post a Comment