Picha zilizonaswa na mtambo wa satellite
Serikali ya Uchina imechapisha picha
zilizonaswa na mtambo wake wa satelite zikionyesha mabaki ya kitu kipana
kikielea katika bahari ya Kusini mwa Uchina.Picha hizo zilipigwa siku
ya Jumapili, saa ishirini na nne baada ya ndege ya abiria ya Malaysia
kutoweka ikiwa na abiria 239, lakini haijabainika ikiwa vifaa hivyo ni
vya ndege hiyo.Huku ikiwa na raia wake 154, ambao walikuwa abiria kwenye
ndege hiyo ya Malaysia, serikali ya Uchina imetuma mitambo kumi ya
satellite kusaidia katika harakati za kutafuta ndege hiyo.Picha za vifaa
hivyo vitatu, ambavyo moja ina upana wa takriban mita 24 kwa 22,
zilichukuliwa siku ya Jumapili, siku moja tu baada ya ndege hiyo
kupotea, lakini zilichapishwa siku ya Jumatano.
Picha zilizonaswa na mtambo wa satellite
Ubawa wa ndege hiyo iliyopotea ina upana wa mita sitini na moja.Picha hizo za satellite zimeweka vifaa hivyo takriban maili mia moja kutoka kwa njia iliyotarajiwa kutumiwa na ndege hiyo na sio mbali kutoka kwa kisima kimoja cha mafuta, ambako mfanyakazi mmoja aliripoti kuona kitu kilichokuwa kikichomeka angani siku ya Jumamosi asubuhi.
Lakini siku chache zilizopita, kumekuwa na fununu kadhaa kuhusiana hatma ya ndege hiyo lakini zote zimekuwa uongo.
Makundi ya uokozi hiyo vile vile wanatafuta mabaki ya ndege hiyo katika maji inayokaribiana na rasi ya Malaysia, kwa sababu wanaamini kuwa ndege hiyo ya Malaysia ilibadili mkondo na kuelekea Magharibi.
Picha zilizonaswa na mtambo wa satellite, mahali inaposadikiwa kuwepo kwa ndege hiyo iliyo potea.
Jitihada zinazoendelea katika utafiti wa ndege hiyo.
(J.G)
0 comments :
Post a Comment