Kupitia Kampuni yake ya ndauka Entertainment msaani wa Filamu Rose Ndauka ameanzisha kampeni ya Ng'arisha Tanzania amabyo inahamasisha kuweka mazingira ya jiji katika hali ya usafi na kupendeza na pia kutunza mazingira, kampeni hii itahusisha kufagia baadhi ya mitaa katika manispaa ya ilala, kuzoa taka na kuzitupa maeneo husika au kuziteketeza huku akishirikiana na kampuni ya Green Waste Disposal.
Rose ndauka akiwa na Abdallah Mbena wakiwa wanaelezea Kampeni hio kwa waandishi wa habari |
"Kwa kuwa jukumu la usafi katika miji linafanywa na mamlaka husika, lakini pia kufanya usafi ni jukumu la kila raia hasa katika maeneo tunayoishi na kufanyia shuguli zetu za maisha. Pia ni jukumu letu sote kuhakikisha kuwa hatuwi chanzo cha kuweka miji katika hali chafu kwa kutupa taka taka hovyo. Tunapokuwa na miji safi inafanya raia wajisikie vyema katika shughuliza na pia kuvutia watalii wa ndani na nje." alisema Rose Ndauka
Kutokana na hayo mimi kama msanii wa filamu na nikiwa kama kioo cha jamii nimeona ni vema kwa kushirikiana na viongozi , raia wa kanda mbalimbali na mamlaka husika kuendesha kampeni hii ya NG'ARISHA TANZANIA siku ya JUMAMOSI TAREHE 15/3/2014 KESHO, kuanzia SAA MOJA aubuhi hadi saa 5 asubuhi amabapo wahusika wote tutakuwa na tutasafisha mtaa wa lumumba katika manispa ya Ilala ikiwa ni ishara ya kuhamasisha raia wote KUAMKA NA KUBADILIKA na kuonyesha mapenzi ya kuweka miji katika hali safi kwa kusafisha maeneo wanayoishi na mitaa na kuzoa taka na kuzitupa au kuziteketeza sehemu husika bila kuharibu mazingira ambapo tumetengeneza jiko kubwa la kuchoma taka.
Rose Ndauka aliendeea kwa kusema, "Faida kubwa ya kuweka miji yetu katika hali ya usafi ni pamoja na kujiepusha magonjwa na kero zinazotokana na uchafu ikiwa ni pamoja na magonjwa ya tumbo, kuhara, kipindupindu, maambukizi yatokanayo na uchafu, kuumizwa na baadhi ya taka, kero ya harufu chafu, kero ya mainzi nk."
Hapo Rose ndauka akifanya usafi maeneo ya Kariakoo siku zilizopita |
kwa mujibu wa takwimu zilizopatikana katika manispaa ya Ilala taka zinazozalishwa ni Takribani tani 1100kwa siku wakati uwezo wa kuzoa taka na kuzitupa ni tani 600 tu. Hii ina maana tani takribani 500 hubaki kila siku. Hii ni sawa na tani zaidi ya 15,000 kwa mwezi au tani 180,000 kwa mwaka. Halikadhalika hali ya usafi katika miji mikuu mingi ya mikoa na wilaya si nzuri. hakika hili ni tatizo kubwa sana na kama sisi wenyewe kama raia hatutabadilika na kujihusisha katika kufanya usafi na kutunza mazingira, basi hali itazidi kuwa mbaya sana." aliongezea Rose Ndauka
Rose Ndauka kupitia kampuni yake ya ndauka Entertainment alimalizia kwa kusema, "Kupitia kampeni ya AMKA NA BADILIKA, NG'ARISHA TANZANIA, napenda kuwaomba watanzania wezangu wa kanda mbalimbali na wenye mapenzi mema kwa nchi yetu tujitokeze kufanya iwe tabia ya sehemu ya maisha yetu kila siku kama vile kuoga na kuvaa nguo safi. kwa upande wangu niko tayari kufanya kazi na taasisi yoyote au mamlaka yoyote katika kuendelea kuhamasisha watanzania kufanya usafi katika miji na makazi yao na kutunza mazingira.
Kampuni ya WASTE DISPOSAL kupitia Manager wao wa Operations Mr Abdallah Mbena amewahakikishia watanzania kwamba kampuni hio ambayo inajuhusisha na uzoaji taka wata shirikiana na Rose ndauka katika kampeni yake hio
Rose Ndauka akiwaonesha waandishi wa habari jiko hilo amabalo kazi yake ni kuchoma TakaTaka |
Rose Ndauka pia alionesha jiko ambalo ametumia zaidi ya Laki Nne kulitengeneza
" jiko hili amabalo kazi yake ni kuchoma taka hata kama ikiwa mbichi au kavu, Jiko hili linatumia mkaa na linaweza kuchoma taka nyingi zaidi uwezavyo." alieleza Rose Ndauka
0 comments :
Post a Comment