.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

Mama wakimarekani aingiza gari baharini akiwa na watoto watatu kwa nia yakuwaua,stori ipo hapa

imeandaliwa na Feisal Pinto
Daytona Beach, Marekani

Mama mjamzito ambae alidiriki kuwachukua watoto wake watatu na kuwaweka kwenye gari na kisha  kuingiza gari hilo kwenye bahari kwa nia ya kujiua pamoja na watoto wake


Mtandao wa Wesh.com ulilipoti kwamba Familia ya mwanamke huyo ilipiga simu kituo cha polisi cha Daytona kueleza jinsi mwanamke huyo alivyokua anafanya mambo ya ajabu masaa machache kabla ya tukio hilo kutokea


Mashahidi walioshuhudia tukio hilo lilotokea katika bahari ya Daytona walitoa maelezo yao na kusema kwamba walisikia sauti za watoto wakipiga makelele, watoto wakike wawili na wakiume mmoja ambao walikadiliwa kuwa na miaka 9 na 10 wakipiga kelele za kwamba mama yao alikua anataka kuwaua


Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 36 kutoka kusini mwa mji wa carolina hivi sasa yupo kwenye moja ya hospitali mjini Florida akiendelea kuangaliwa kama anamatatizo ya akili.



Askari wanasema lazima kutakua na ugonjwa uliomfanya mwanamke huyo kuendesha gari mpaka baharini

Tim Tesseneer kutoka Rutherfordton, magharibi ya Carolina ameiambia mtandao wa WESH 2 kwamba yeye alikua miongoni mwa watu wakwanza walioenda kuwaokoa watoto hao pindi mama yao alipo acha barabara na kuingia Baharini

"Watoto wawili walikua wamekaa siti ya nyuma walikua wakilia kwa nguvu huku wakisema "Mama anataka kutuua,tusaidieni" huku mikono yao ikiwa nje" alisema Tim Tesseneer

Video ambayo ipo chini inaonesha mmoja wa waokoaji akiwa amewabeba watoto wawili waliotolewa kwenye gari hilo lililokua linazama, ndipo watoto hao wawili wakawaambia kwamba yupo mtoto mwingine kwenye gari hilo.

'watoto hao walisema, "hapana kuna mtoto mwingine. kuna mtoto," 'Aliongezea Mr Tesseneer. 'Mwanamke huyo(mama wa watoto hao) hakusema chochote kuhusu mtoto aliebaki ndani ya gari hilo'
"Mama huyo alikua na muonekano flani ambao siwezi kuelezea. ulikua muonekano wa aibu na uwoga " alisema shuhuda huyo


kwenye video iliochukuliwa na Simon Besner Mtalii kutoka Canada, alimuonesha mwanamke huyo akiwa nje ya gari hilo huku waokoaji wakiwa wanaendelea kuwatoa watoto hao kwenye gari hilo

Mashuhuda wanasema mama huyo alitokea dirishani huku watoto wake wakibaki kwenye viti vyao wakiwa bado wamefungwa mkanda.



Mtalii mwingine alielezea tukio hilo la ajabu
"Rafiki yangu alinionesha gari hilo likiwa linaelekea baharini, kisha kumuona mtoto akitoa mikono nje akipiga kelele za kuomba msaada huku gari likiendelea kwenda baharini, ndipo hapo nilipomuona kijana akilikimbilia gari hilo na kisha kuwatoa watoto wawili, ndipo kijana mwingine akaingia kwenye gari hilo na kumtoa mtoto mdogo aliekua amebaki ndani ya gari hilo"

Mashuhuda wengi walichangania na kusema yakwamba hamna uwezekano wowote ule kwamba tukio lile lilikua sio la kukusudia labda kama ana matatizo ya akili..

Watoto hao watalelewa na ndugu mara baada yakutoka hospitalini ambapo wanatibiwa majeraha madogo madogo 

Gari hilo lilipotelea baharini, Askari ndio watakua na maamuzi yamwisho kama mama huyo atahukumiwa au laa
Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad