.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

MJUE KOCHA MPYA ALIECHAGULIWA NA TFF.





 

Tangu TFF kusema inatafuta kocha mpya atakayerithi mikoba ya Mdenmark, Kim Poulsen, mtandao huu umekuwa ikifuatilia kwa undani mwalimu mpya wa Stars atakuwa nani na sasa inaibuka na jibu ni Mart Nooij.

Tayari Nooij ambaye kwa sasa ni kocha wa St George ya Ethiopia amekwishasaini Mkataba wa miaka miwili na TFF na atakuja nchini mwishoni mwa mwezi huu.

Nooij amekua mwalimu wa maendelo katika taasisi ya Mpira ya Royal Dutch. Huku akiwa amefanya kazi EVC mwaka 1913 nchini Marekani na Kazakhstan. Pia alishawai kuwa kocha wa timu ya mpira ya Burkina Faso chini ya miaka 20 wakati timu hio ilipokua inashiriki Mashindano ya Vijana mwaka 2003. Huku mwaka 2004 alichaguliwa kuwa kocha msaidizi wa muda wa FC Volendam.

Mnamo mwaka 2007 alichaguliwa kuwa kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Mozambique, akiwa kocha wa Mozambique aliweza kupeleka timu hio kushiriki komba la mataifa ya Africa 2010. Mozambique alimaliza mashindano hayo ikiwa yamwisho kwenye kundi lao ikiwa imetoa draw mechi moja na kufungwa mechi 2. Baada ya kushindwa kufika hatua ya mbali kwenye mashindano hayo Kocha huyo alijiuzuru mwezi wa tisa 2011, Nafasi yake ikachukuliwa na mjerumani Gert Engels.

19/4/2012, alitajwa kuwa kocha mkuu wa Santos inayocheza lgi kuu South Africa, na kisha kufukuzwa tarehe 18/12/2012 na St George ya Ethiopia anakoendelea na kazi hadi sasa.
Baada ya kusaini Mkataba wa miaka miwili na TFF kuja kuifundisha Stars, Nooij anasubiri barua maalum ya kuruhusiwa kuondoka baada ya kukamilisha taratibu za kuvunja Mkataba uliokuwa unaelekea ukingoni na klabu hiyo ya Addis Ababa. 
Yanga SC pia inafundishwa na kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm.


Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad