MADRID, Hispania
MSHAMBULIAJI Cristiano Ronaldo amemlaumu mwamuzi wa mchezo wao wa juzi dhidi ya Barcelona, Alberto Undiano, akimtaja kuwa chanzo cha wao kuchapwa mabao 4-3.
Mchezaji huyo wa Real Madrid, alisema: "Mwamuzi alifanya makosa mengi. Tunahitaji kuwa na mwamuzi ambaye ana kiwango cha juu kama mchezo wenyewe. Alionekana dhaifu na mwenye hasira. Sitaki kuzungumzia matokeo, lakini mwamuzi aliboronga."
Mchezaji huyo bora wa dunia 'Balon d’Or', pia alisema kuhusu timu yao kuchukiwa, aliongeza: "Kuna watu ambao hawataki kuona sisi tukishinda, na hawataki kuiona Barcelona ikitolewa katika mbio za ubingwa.
"Inawakera baadhi wakiona Madrid inashinda. Watu wanakereka. Hali si kama ya zamani. Watu wanataka Barcelona kubaki katika mbio za ubingwa na hilo ndilo linalowafanya kuendelea kubaki."
Cha ajabu hakukuwa na maneno kama hayo ya kumshambulia mwamuzi kutoka kwa Kocha wa Madrid, Carlo Ancelotti, ambaye alisema ushindi wa Barcelona ulitokana na mshambuliaji Lionel Messi na si mwamuzi.
Kikosi cha Ancelotti sasa kimebakiza tofauti ya pointi moja kutoka kwa Barca katika msimamo wa Ligi Kuu Hispania, ambapo michezo 12 imebaki.
Mwamuzi alibadilisha mchezo hasa katika kipindi cha pili wakati alipoamua upigwa mkwaju wa penalti akisema Neymar alichezewa vibaya na Sergio Ramos, ambapo alitoa penalti na kadi nyekundu.
Lakini Ancelotti alisema: "Sikuangalia kwa mara ya pili tukio lile, hivyo siwezi kusema kama mwamuzi amesababisha sisi kupoteza mchezo huu. Hicho si kitu ambacho nilizungumza na wachezaji baada ya mchezo."
Hat-trick ya Messi ilikuwa ni pigo kubwa kwa Real Madrid, na Ancelotti alisema: "Kama unafanya makosa mbele ya Messi, siku zote anakuumiza."
source: JamboLeo

0 comments :
Post a Comment