Yawezekana maisha ya Victor Valdes ndani ya Barcelona yakawa ndo yamefika Ukingoni, Valdes ambae ni kipa namba moja wa Barcelona ambae kwa sasa ni majeruhi.
| Wachezaji wa Barcelona wakimuangalia Kipa wao baada kuanza kupiga kelele za maumivu |
Valdes alipatwa na Majeruhi wakati timu yake ya Barcelona ilipokutana na Celta Vigo usiku wa Jumatano, Madaktari wa timu hio wamesema valdes anahitajika kufanyiwa upasuaji wa goti baada ya kuumiza misuri ya ndani baada kutua vibaya alipokua akiokoa mpira katika dakika ya 23.
Valdes alitolewa nje ya Uwanja katika dakika ya 23 huku akionekana na maumivu makubwa sana.
| Victor Valdes akitolewa Nje ya uwanja baada ya Jeraha hilo |
Barcelona kupitia mtandao wao wameandika 'Valdes aliumia goti baada ya kutua vibaya akiwa anaokoa faulo iliopigwa na Augusto.
'Madaktari wamesema Valdes aliumia goti lake la kulia na kumfanya aombe kutolewa nje ya Uwanja'
| Valdes akionekana mwenye maumivu wakati akitolewa nje ya Uwanja |
Valdes ambea alijuinga na barcelona akiwa na miaka 10, na kuanza kuitumikia timu hio 2002 alipelekwa moja kwa moja hospitalini baada ya kutolewa uwanjani huku mchezo huo ukiendelea baada ya kipa namba mbili Pinto kuchukua nafasi yake.
Valdes atakua nje kwa miezi kadhaa huku zikiwa zimebaki mechi 6, pia inajulikana kwamba valdes ataondoka mwisho wa msimu mara tu baada ya mkataba wake kuisha.
| Valdes akionekana mwenye maumivu baada ya kutua wakati akiokoa mpira wa faulo uliopigwa na Augusto |
Barcelona wanaruhusiwa kusajiri golikipa kama usajiri wa mkopo wa dharura kutoka timu yeyote ile katika ligi ya Hispania (La Liga)ila kocha wa timu hio Martino amesema hato sajiri kipa yeyote kwa sasa, na kwamba ataendelea na kundi hilo lililopo sasa.
0 comments :
Post a Comment