Klabu ya
Barcelona sasa inaweza kununua na kuuza wachezaji katika kipindi hiki
cha usajili baada ya Fifa kutupilia mbali adhabu yake iliyotoa kwa klabu
hiyo ya kutosajili.
Miamba hiyo ya Uhispania ilipewa adhabu ya miezi 14 kutonunua wamchezaji baada ya kuthibitika kuvunja sheria kwa kuwasajili wachezaji wa kimataifa walio na umri wa chini ya miaka 18 ingawa sasa adhabu hiyo imetupwa kapuni.
Nahodha wa
klabu hiyo Carles Puyol na mlinda mlango wa muda mrefu Victor Valdes
wametangaza kuitema klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu.
Mabingwa hao
wa Uhispania walikutana na rungu la Kamati ya Nidhamu ya Fifa April 2
mwaka huu kwa kuvunja sheria ambapo waliadhibiwa kutosajili kwa kipindi
cha miezi 14 ingawa waliruhusiwa kuuza wachezaji pekee na kutozwa faini
ya franga za Uswis 450,000.
Baada ya
Barcelona kufuata ahadi ya kukata rufani, Fifa iliamua kwamba kutokana
na uzito wa kesi yenyewe na uwezekano wa kukata rufani katika Court of
Arbitration for Sport (Cas), ikataka kuimaliza kabla ya ufunguzi wa
dirisha la usajili ambalo litafunguliwa rasmi July 1 na kwa hiyo ikatupa
kapuni adhabu hiyo.
Sheria za Fifa zinaeleza kwamba
uhamisho wa kimataifa unaruhusiwa tu kwa wachezaji waliokuwa na umri wa
zaidi ya miaka 18 - au mchezaji husika awe na sababu kuu tatu.
Mchezaji wa
chini ya umri wa miaka 18 anaweza kuhamia kwenye klabu ya nchi nyingine
kama wazazi wake watakwenda nchini humo kwa sababu zisizokuwa na
kimpira, au kama wanatoka katika nchi nyingine ambayo ni mwanachama wa
Umoja wa Ulaya au Jumuia ya Uchumi ya Ulaya na awe na umri kati ya miaka
16 na 18, au wanaishi ndani ya 100km za klabu.
0 comments :
Post a Comment