Baada ya nyimbo zake kufanya vizuri sana katika nchi za Afrika
Mashariki, Diamond Platnumz ameonekana kukubalika na nchi za Afrika
Magharibi. Habari nzuri ni kwamba
Diamond amepata shavu la kushirikishwa katika wimbo wa mwandadada Waje.
Waje ni msanii anaefahamika sana kwao Nigeria na moja kati ya wimbo
uliyomtambulisha sana ni ule aliyoshirikishwa na P-square ulijulikana
kama Do Me (2008).
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Waje aliandika ujumbe huu kmhusu
Diamond, ”Met this amazing brother yesterday, humble nd such an
inspiration,his work ethic is super. #africanlegendsmakingmusic
@diamondplatnumz the talent eh. Thanks so much for this honour”
Diamond aliondoka Tanzania wiki ijayo kwenda Nigeria ambapo anatarajia
kufanya kolabo na wasanii mbalimbali kutoka Nigeria na Ghana. Kolabo ya
My Number One aliyofanya na Davido ndio imemtambulisha sana Afrika
Magharibi.
Source: JestinaGeorgeBlog
0 comments :
Post a Comment