BONDIA Ronald Pontillas, amewasili nchini leo asubuhi kwa ajili ya pambano lake la kimataifa dhidi ya bondia Francis Miyeyusho,
litakalofanyika Jumamosi kwenye Ukumbi wa PTA, Dar es Salaam.
Akizungumza Dar es Salaam juzi, mratibu wa pambano hilo Mussa
Kova, alisema kuwa Pontillas raia wa Ufilipino, atawasili nchini
akiwa na kocha wake Amogo Samson.
Kova alisema bondia huyo amewasili majira ya saa moja asubuhi,
kutumia ndege ya Qatar Airways.
Amesema kuwa moja kwa moja amefikishwa hotelini kupumzika kabla ya saa 5, kuzungumza na vyombo vya habari.
Kova alisema kuwa maandalizi mengine yanaendelea vizuri
ambapo, hata suala la viingilio nalo tayari
limeshapangwa.
Alisema katika viingilio vitakuwa vya aina mbili ambavyo ni
sh.20,000 kwa VIP na kawaida itakuwa sh.10,000.
Alisema kuwa katika pambano hilo kutakuwa na mapambano ya
utangulizi ambayo atayatangaza katika mkutano maalum na
vyombo vya habari.
Pia Kova alisema maandalizi yanakwenda vizuri na
kusisitiza kuwa litasimamiwa na chama cha
ngumi za kulipwa Tanzania (PST).
kusisitiza kuwa litasimamiwa na chama cha
ngumi za kulipwa Tanzania (PST).
"Mabondia wote wako katika hali nzuri ya ushindani, tunategemea
Miyeyusho atafanya vizuri na kukabiliana na upinzani wa
mpinzani wake kwani ni bondia mzuri na mwenye kiwango cha
juu," alisema
Kova.
Kova.
0 comments :
Post a Comment