Kijana aliyefahamika kwa jina la Samson Ntemi aliyetuhumiwa kwa utapeli wa madini bandia
MTU mmoja
aliyefahamika kwa jina la Samson Ntemi (44) mkazi wa Msingwi, Wilaya ya
Magu mkoani Mwanza amenaswa na Polisi wakati akifanya jaribio la
utapeli wa madini feki huko Kijitonyama jijini Dar es Salaam hivi
karibuni. Kwa mujibu wa chanzo makini, mtu huyo alianza harakati za
utapeli wake kwa kumpigia simu mfanyabiashara mmoja wa magari akimweleza
kuhusu nia yake ya kununua gari aina ya Canter kutoka kwake kwa kiasi
cha shilingi milioni 32.
Chanzo
kilisema kufuatia simu mfululizo za mtu huyo, mfanyabiashara huyo
alipata hofu na kuhisi huenda alikuwa ni tapeli, hivyo kuweka mtego na
kumtaka wakutane Mwananyamala kwa ajili ya kufanya biashara hiyo. Lakini
hata hivyo, walipokutana tapeli huyo alimtaka mfanyabiashara huyo
kuongozana naye hadi Kurasini, akidai ndipo alipokuwa mteja mwenye
kulihitaji gari hilo.
Nilipomhoji vizuri akaniambia yeye ni
mfanyabiashara wa madini kutoka Mahenge, Ifakara, mkoani Morogoro
aliyefika Dar kutafuta soko huku akionesha kutolijua vizuri Jiji la
Dar,” chanzo chetu kilimnukuu mfanyabiashara huyo akisema.
Inadaiwa kuwa tapeli huyo alimwonyesha
mfanyabiashara huyo madini hayo yenye thamani ya mamilioni ya shilingi
na kumtaka anunue. Baada ya kuyaona na kugundua kuwa ni feki, alimtaka
tapeli huyo kuandamana naye hadi benki maeneo ya Kijitonyama ili
amkabidhi.
Ads by OnlineBrowserAdvertisingAd Options
About feisal pinto
Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
0 comments :
Post a Comment