Wababe wa soka wa Hispania Barcelona wanajianda kutangaza dau jipya kwa ajili ya kumsajili Luis Suarez kutoka katika timu ya Liverpool.
Wanatarajia kutoa dau la euro milioni 88 zinazohitajika na Liverpool, mara baada ya dau lao la kwanza linalokaribia euro milioni 82 kupigwa chini.
Mabosi wa Liverpool pamoja Barcelona walikutana Jijini London siku ya Jumatano, ambapo timu hiyo ya Catalunya ilitoa dau la euro milioni 82 wakati huo Alexis Sanchez akitumika kama sehemu ya makubaliano ya kubadilishana wachezaji.
Inasemekana wababe hao wa Hispania wana mpango wakuboresha mazungumzo na Liverpool ili wamalizie usajili huo mara baada ya mkutano wao wa Jumatano kuanza kuzaa matunda .
Liverpool bado wapo katika mbio za kumsajili Sanchez ambaye Barcelona wameamua kumuondoa kama sehemu ya makubaliano ya kubadilishana wachezaji na timu hiyo kutoka Anfield, Arsenal wanaonekana kuziongoza mbio hizo,
Wamiliki hao wa Liverpool wanaojulikana kama Fenway Sports Group wamesisitiza kuwa hawatamruhusu Suarez ahamie Nou Camp kama Barcelona watashindwa kufikia angalau dau la euro milioni 88, ikiwa kama ni ada iliyopo kwenye mkataba wao na Suarez kwa timu itakayo taka kumsajili.
Baada ya maboresho ya mkataba yaliyofanyika mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka 2013, ambapo Suarez alikuwa akilipwa euro 283,000 kwa wiki.
0 comments :
Post a Comment