Unajua kwa nini baadhi ya timu zinazoshiriki ama zilizoshiriki Kombe la Dunia la FIFA huwa na nyota kadhaa kwenye nembo za vyama vyao vya kabumbu?
Timu hizo huweka idadi ya nyota sawasawa na idadi ya mataji ya ubingwa wa dunia
wanayoyashikilia. Hivyo, nyota hizo, huwa nishani ama heshima kwa kutambua ubingwa wa nchi husika.
Brazil huweka nyota tano kwa kuwa ndiyo idadi ya mataji ya kombe la dunia inayoyashikilia. Timu za Ujerumani, Ufaransa, Argentina na Uingereza nazo huweka nyota sawasawa na idadi ya mataji yao.
Wadadisi wengine wanaweza kustaajabishwa na jezi ya Uruguay yenye nyota nne ilhali ni wazi wameshinda kombe la dunia mara mbili tu, 1930 na 1950. Jibu ni kuwa, nyota mbili zingine zinawakilisha ubingwa wa michuano ya Olimpiki ya mwaka 1924 na 1928 ambayo FIFA inautambua ubingwa wake kama ubingwa wa dunia.
Kuvaa huko kwa jezi zenye nyota hakujatokea tu. Kunatokana na Kifungu cha 18.2 cha Kanuni za Vifaa za FIFA. Kifungu hicho kinaruhusu wanachama wa FIFA waliowahi kushinda kombe la dunia kuweka alama kwenye jezi zao kama kielelezo cha ushindi huo.
Si hivyo tu, vilabu kadhaa vya soka ulimwenguni pia huweka nyota kama kielelezo cha mafanikio yao katika kabumbu. Nottingham Forest ya Uingereza huweka nyota mbili kutokana na mafanikio yao
0 comments :
Post a Comment