.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

TUTATOBOA BILA NEYMAR -SCOLARI


scolari_bdcf2.jpg
Kocha wa Brazil Luiz Filipe Scolari amesema vijana wake wataweza kucheza bila ya mshambuliaji wake aliyeumia, Neymar, watakapocheza na Ujerumani siku ya Jumanne katika nusu fainali ya Kombe la Dunia.
Neymar amepachika mabao manne kati ya manane yaliyofungwa na Brazil katika michuano hiyo, lakini hatoweza kuendelea kucheza baada ya kuumia uti wa mgongo katika mchezo wa robo fainali dhidi ya Colombia.
Scolari amesema kikosi chake kiko makini na shughuli inayowakabili.
“Neymar ametekeleza sehemu ya wajibu wake. Sasa ni juu yetu kutekeleza majukumu yetu,” amesema kocha huyo.
“Tumekubaliana na yaliyotokea na tutaelekeza nguvu zetu katika masuala mengine. Katika mechi hii, hatutakuwa tunacheza kwa ajili yetu tu, bali ndoto zetu na pia kwa ajili ya Neymar na kila alichotufanyia.”
Brazil inacheza na Ujerumani saa tano usiku Afrika Mashariki.
BBCSWAHILI
Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad