.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

DKT. JOHN MAGUFULI AWAZIBA WATU MIDOMO KWA KUENDELEA KUTIMIZA AHADI ZAKE, CHEKI HII SASA

PICHA: Taswira mbalimbali zikionyesha Kivuko cha MV.Dar es Salaam kikiwa kimeshushwa majini leo tayari kwa kuanza safari ya kuja Tanzania.
Ile ahadi ya Waziri wa Ujenzi Dkt.John Magufuli ya kununua kivuko kipya kitakachotoa huduma ya usafiri kati ya Jiji la Dar es Salaam na mwambao wa Bahari ya Hindi hadi Bagamoyo imetimia. Taarifa za uhakikia tulizozipata hivi punde ni kuwa kivuko hicho (Mv Dar es Salaam) kilichokuwa kinajengwa na kampuni kutoka Denmark leo kimeshuka majini na tayari kuanza safari ya kuja Dar es Salaam ambapo kinatarajiwa kufika/kutua Dar es Salaam kati ya wiki tatu mpaka nne zijazo.
Kivuko cha MV Dar es Salaam kitakuwa na kasi kuliko kivuko chochote Afrika ya Mashariki na hasa mwambao wa bahari ya Hindi ukiacha Afrika ya Kusini.
Kivuko hiki ni muendelezo wa juhudi za Wizara ya Ujenzi za kupunguza msongamano katika Jiji la Dar es Salaam ikiwa ni pamoja na kujenga barabara za New Bagamoyo (Kawawa JCT - Tegeta); ujenzi wa miundombinu ya mabasi yaendayo haraka (Bus Rapid Transit Infrastructure - BRT) ikiwemo kuanza ujenzi wa miundombinu ya mabasi yaendayo haraka awamu ya pili ; ujenzi wa ‘Flyover’ ya TAZARA na UBUNGO ; barabara za pete (DSM Outer Ring Roads); barabara ya Dar es Salaam – Chalinze Expressway; kupanua barabara ya lami sehemu ya Gerezani (KAMATA – Bendera Tatu) kutoka njia mbili za sasa hadi njia nne; kujenga daraja la Kigamboni linalounganisha Kurasini na Kigamboni, daraja hili linatarajiwa kukamilika mwakani mwezi wa sita.

ANDIKA MAONI YAKO CHINI TAFADHALI
Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad