Wanachama na mashabiki wa Simba Sports Club wakiwa katika picha na Rais wao, Evans Elieza Aveva (aliyevalishwa shada la ua) katika uzinduzi wa tawi la klabu hiyo mkoani Mtwara
Na Mwandishi Wetu, Mtwara
WEKUNDU wa Msimbazi, Simba Sc leo jioni wanacheza mechi ya kirafiki na Ndanda fc katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara katika maadhimisho ya Siku ya Ndanda, ‘Ndanda fc Day’. Wakati kikosi cha Simba kikitarajia kutua asubuhi ya leo Uwanja wa Ndege wa Mtwara kutokea Dar es salaam , jana Rais wa klabu hiyo, Evans Elieza Aveva akiongozana na mwenyekiti wa zamani wa klabu hiyo, Hassan Dalali walitua Mtwara kwa ajili ya maandalizi ambapo kikubwa zaidi alizindua Tawi jipya la Simba mkoani humu.
Simba jana ilikuwa na mechi ya pili ya kimataifa ya kirafiki katika uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam dhidi ya URA ya Uganda na ilifungwa bao 1-0. Wikiendi iliyopita ilishinda mabao 3-0 dhidi ya Gor Mahia ya Kenya katika mechi ya kwanza ya kimataifa ya kirafiki.
Wakati Ndanda fc imepanda Daraja, mapokezi ya timu hiyo hapa Mtwara ambapo walizindua ‘Slogani’ yao kuwa ‘Ndanda fc kwanza, Simba, Yanga baadaye’, lakini jana mashabiki hao waligeuka na kusema haiwezekani, ‘Simba kwanza, Ndanda fc baadaye’.
Walipobanwa na mwandishi kwanini wamegeuka? walijitetea na kusema mechi ya leo ni ya kirafiki ndio maana wanaishangilia timu yao ya Simba, lakini vijana hao wa Patrick Phiri wakirudi katika mechi ya ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara watakutana na mambo mapya na hapo ndipo ‘Ndanda fc itakuwa kwanza, Simba baadaye”. Raha sana.
Zaidi walisema wamefurahishwa na ujio wa Rais wao wa kwanza katika Historia ya klabu hiyo, Bwana Aveva, hivyo wamempokea kwa furaha na wanaandika historia ya kuzindua tawi jipya.
Msomaji unaweza kupata picha mwenyewe kuhusu namna mashabiki walivyo inapofika Simba na Yanga.
Hapa chini ni baadhi ya picha katika mapokezi ya Aveva na uzinduzi wa tawi…
Jamaa kavalia jezi yenye jina la Emmanuel Okwi: Mambo yalianza mdogo mdogo baada ya Rais wa Simba, Evans Aveva kuwasili mkoani Mtwara akitokea Dar es salaam
Tawi la Mnyama mkoani Mtwara
Umeona nini kwenye picha hii? kuna jamaa kavalia jezi ya timu pinzania, hakuona shida kuwaona watani. Lakini ni ngumu kufahamu, labda kavaa tu kama vazi. Cheki kofia nayo…..
Wamegeuka?: ‘Simba kwanza, Ndanda fc baadaye’., mashabiki wa Simba wakati wa uzinduzi wa tawi la klabu hiyo Mkoani Mtwara
Rais wa Simba (wa pili kulia) wakati wa kusaini kitabu cha wageni kwenye tawi hilo. Wa kwanza kulia ni mwenyekiti wa zamani wa klabu hiyo, Mzee Hassan Dalali.
Rais wa Simba sc, Evans Aveva (wa kwanza kushoto) na Hassan Dalali (wa kwanza kushoto) wakipata msosi kidogo
0 comments :
Post a Comment