Usiku wa jana kwenye ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam, Tanzania imempata mrembo ambaye atawakilisha vyema nchi katika mashindano ya Miss World yatakayo fanyika hapo mwakani.
Sitti Abbas Mtemvu ni Miss Tanzania 2014 akiwa katika pozi na mshindi wa pili, Lillian Kamazima (kulia) pamoja na mshindi wa tatu, Jihhan Dimachk baada ya kutangazwa mshindi.
MREMBO Sitti Mtemvu kutoka Temeke ametwaa taji la Miss Tanzania 2014 na kujinyakulia kitita cha milioni 18 usiku huu katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Nafasi ya mshindi wa pili imekwenda kwa Lilian Kamazima ambaye amejishindia shilingi milioni 6 huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na Jihan Dimachk. Dorice Mollel ameshika nafasi ya nne wakati Nasreen Abdul akichukua nafasi ya tano.
Kwa ushindi huo, Sitti atapeperusha bendera ya Tanzania katika mashindano ya Miss World 2015.
Pichani ni Washiriki waliochaguliwa kuingia kwenye hatua ya tano bora katika shindano la Redds Miss Tanzania 2014 linaloendelea hivi sasa ndani ya ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar.
Mmoja wa Washiriki waliongia katika nafasi ya tanno bora shindano la Redds Miss Tanzania 2014 wakijibu maswali mbalimbali.…
Pichani ni Washiriki waliochaguliwa kuingia kwenye hatua ya tano bora katika shindano la Redds Miss Tanzania 2014 linaloendelea hivi sasa ndani ya ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar.
Mmoja wa Washiriki waliongia katika nafasi ya tanno bora shindano la Redds Miss Tanzania 2014 wakijibu maswali mbalimbali.
Msanii wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz akitumbuiza jukwaani akiwa na Vanessa Mdee mbele ya wageni waalikwa (hawapo pichani),waliofika kushuhudia shindano hilo.
Msanii wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee ‘V-Money’ akitumbuiza kwenye shindano la kumsaka mshindi wa Redds Miss Tanzania 2014,yanayofanyika usiku huu ndani ya moja ya ukumbi wa Mlimani, jijini Dar.
Baadahi ya Wageni waalikwa wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye shindano hilo la kumsaka Kinara wa Redds Miss Tanzania 2014.
Washiriki wa Shindano la Redds Miss Tanzania 2014 walicheza moja ya onesho lao la ufunguzi wa shindano hilo, ambapo mshindi alijinyakulia kiasi cha shilingi miloni 18 taslim.
0 comments :
Post a Comment