Angelina Jolie kwa sasa anafilamu mbili anazozifanyia kazi Unbroken na By the Sea .Muigizaji huyo wa Hollywood kwa sasa ndie nyota wa majarida mawili Variety na DuJour
Katika mahojiano yake na jarida la DuJour Angelina alizungumzia jinsi anavyofanyakazi na mumewe Brad pitt kwenye scene tofauti
Kuhusu swala la kuacha kuigiza Angelina alisema
“Sikuwahi kupenda kuwa mbele ya Camera wala sijawahi kufikiria kuongoza filam ila natumai kuwa na fani hii kwa sababu ninaifurahia saana”
pia alizungumzia jinsi anavyofanya filam ya By sea akiwa na mumewe
Angelina alidai anakutana na changamoto nyingi pale anaposimama kama muongozaji kumuongoza mumewe lakini pia kujiongoza mwenyewe, aliongeza kuwa sio kazi rahisi kwake lakini anafuraha kwa sababu changamoto ni kitu kizuri kwake
Akizungumzia kuhusu filam ya Unbrocken na watoto wake alisema alikuwa anahitaji kutengeneza filam ambayo itawaisaidia watoto wake kuwa wanaume bora
Source: EFM WEBSITE
0 comments :
Post a Comment