.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

Serikali: "Mara Kaskazini haina vigezo vya kuwa mkoa."

Serikali imesema haiwezi kuutangaza mkoa wa Mara Kaskazini kutokana na kutokidhi vigezo na utaratibu unaostahili kutangazwa kuwa mkoa.
Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Uratibu na Bunge, Mhe. William Lukuvi

Akijibu swali la mbunge wa Tarime, Mh. Nyambari Chacha Nyangwine je ni lini wilaya za Tarime na Rorya zitatangazwa rasmi kuwa mkoa wa Mara Kaskazini kutokana na ukubwa wa jimbo la Tarime.
Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Uratibu na Bunge, Mhe. William Lukuvi amesema tume ya taifa ya uchaguzi inatarajia kutoa mwongozo kwa makatibu tawala wa mikoa na wakurugenzi wa halmashauri zote nchini kuhusu vigezo na utaratibu wa kuzingatia katika kuwasilisha maombi ya kugawa jimbo kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Amesema maombi yote ya kuanzisha mkoa mpya ni lazima yajadiliwe kwenye vikao vya kisheria vya mkoa na wakishakubaliana na hutakiwa kuwasilisha maombi husika Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa baada ya uchambuzi wa waziri mkuu umshauri Rais ambaye ndiye mwenye dhamana na mamlaka husika.
Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad