Kuna ule msemo usemao "Asiefanya kazi na asile" ila anaefanya kazi atambulike na apewe credits zake.
Yawezekana umeshawahi kusikia Jina la "Didas" popote tu way back 2004 tangu enzi za "Didas health Care" , kisha "Didas Fashion" ila kwa sasa "Didas Entertainment" ndo jina linalotumika na kwa sasa wamesha fungua Radio nchini Tanzania.
Pia Ukiongelea promoters wanao wapeleka wasanii wa Bongo wakafanye show nje ya nchi basi "khadija seif" ambae anajulikana kama "Didas" pia ndo mmiliki wa "Didas Entetainment" ni miongoni wao, Kupitia mtandao wa kijamii Facebook na Instagram mmiliki wa Didas Entertainment, khadija seif (Didas) amefunguka hivi
"Asante mungu siku zote mwanzo huwa mgumu, ila kila anae hangaika kutafuta riziki kwa jasho lake mungu humpa haki yake. Mimi binafsi nakiri kuwa, mwanzo wakati tunaleta wasanii kutoka bongo, wengi walikuwa wakifikia kwenye nyumba zetu, na tulikuwa tuna deal kibongo bongo, ila kutokana na kuwa mtu ujifunza kupitia makosa anayo yafanya, sasa#DidasEntertainment imejifunza makosa mengi sana, basi sasa tumeamua kufanya kazi ki professional na Kuanzia sasa wasanii wetu watakuwa wakifikia kwenye apartment maalum tulizo ingia nazo mkataba na zipo full sponsored. 2015 will be the year for all changes."
0 comments :
Post a Comment