.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

YAMOTO BAND WAWAFARIJI WATOTO YATIMA MAJIMATITU

Displaying ASHA.JPG
TAASISI ya Mkubwa na Wanawe Youth Center, imekakabidhi msaada wa vyakula kwa kituo cha watoto yatima cha Hisani kilichopo Mbagala Majimatitu, Dar es Salaam.


Akizungumza jana mara baada ya kukabidhi msaada huo wa vyakula mbalimbali, ikiwemo unga, mchele, maharage, sukari, mafuta ya kula, soda na maji ya kunywa, Mkurugeni wa Mkubwa na Wanawe, Said Fella, alisema kuwa wamefanya hivyo ni sehemu ya kurudisha kile wanachokipata kutoka kwa jamii.




Fella alisema kwa kutambua mchango wa mashabiki huku naye akiwa  yatima, kutokana na kuwapoteza wazazi wake wote, ameona ni muhimu kutoa msaada huo.
 Alisema yeye kwa kushirikiaana na wenzake wameona kila wanapopata nafasi wachangie hata kidogo ili waweze kusaidia.

"Nami kama yatima nina kila sababu ya kushirikiana na wenzangu kuhakikisha tunachangia hata kidogo tunachopata " alisema Fella ambaye hivi karibuni alitoa msaada kama huyo Shinyanga na kuwataka  wasanii na wadau wengine kukumbuka vituo hivyo.



  Naye msanii wa Kundi la Yamoto Band Asilahi Isihaka 'Dogo Aslay'  aliwaomba watu wengine wenye uwezo kujitokeza kwa kusaidia vituo yatima kwa kuwa hawana uwezo, kwa kufanya hivyo inafanya wajisikie faraja.

Naye Mkurugeniz wa kituo hicho, Hidaya Shukrani, aliwashukuru Mkubwa na Wanawe kwa kuwasaidia.


Alisema kuwa msaada uliotolewa ni mkubwa na kuwaomba naomba wengine kujitokeza kuwasaidia kama walivyofanya mkubwa na wanawe.

Alisema katika kituo hicho kina watoto yatima 40 ambao wengine wanasoma na wengine bado watoto wadogohuku kikiwa na changamoto  nyingi kama sehemu maalumu ya kuishi, hivyo mara nyingi kuhamahama na kuomba wadau pamoja na  serikali iwasaidia makazi maalum.
Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad