Waziri Mkuu mstaafu wa awamu ya Pili Fredrik Sumaye amewatadhaharisha watanzania hasa vijana kuepuka wanasiasa wanaotafuta madaraka kwa kutumia nguvu za ziada kwa kuendesha siasa zenye misingi ya chuki na rushwa.
Waziri Mkuu mstaafu wa awamu ya Pili Fredrik Sumaye
Waziri Mkuu mstaafu wa awamu ya Pili Fredrik Sumaye amewatadhaharisha watanzania hasa vijana kuepuka wanasiasa wanaotafuta madaraka kwa kutumia nguvu za ziada kwa kuendesha siasa zenye misingi ya chuki na rushwa kwani wakishafanikiwa kipaumbele cha kwanza kitakuwa kuendelea kutumia rasilimali za nchi kufidia gharama na nguvu walizotumia.
Akizungumza katika kongamano la kuwawezesha vijana wa sekondari na vyuo vikuu kutambua nafasi yao katika kudumisha amani wakati wa uchaguzi linalofanyika jijini Arusha Sumaye amesema ushindani wa kisiasa wa aina hiyo hauna tija kwa wananchi wala kwa vyama vya siasa badala yake umeendelea kuangamiza rasilimali za nchi na kuwaongezea wananchi umaskini.
Aidha sumaye amesema uzoefu unaonesha kuwa nchi zote zilizoshindwa kulitambua hilo zimeingia kwenye matatizo makubwa na zimeshindwa kuunda serikali inayokubalika na zimeishia kuunda serikali za mseto ambazo pia hazikusaidia badala yake zimeweka makubalino kula kilichopo badala ya kutatua matatizo yaliyopo.
Mratibu wa taasisi inayoelimsha vijana wa sekondari na vyuo vikuu kutambua nafasi zao katika kudumisha amani wakati wa uchaguzi Nikson Mmanyi amewataka vijana kutokubali kutumiwa kutumika vibaya kwa kufanya mambo yanayoivuruga nchi yao.
Kwa upande wao baadhi ya viongozi wa dini akiwemo Shekh wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Shabani bin Juma amesema umakini, uvumilivu na kuzingatia misingi ya haki vinahitajika kwa kiasi kikubwa hasa wakati huu ambao taifa linaelekea kwenye uchaguzi na ni wajibu wa kila mtanzania.
0 comments :
Post a Comment