Mpiga picha maarufu nchini Edwin Elinema maarufu kwa jina la EdwinTza255 amepatwa na mkasa mkubwa hapo jana baada ya kupigwa na msanii ChidyBenz.
Kupitia Ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram, Edwin alieleza yaliomkuta na sababu ya kupigwa na msanii huyo ambae anakesi mahakamani ya kukutwa na dawa za kulevya na misokoto ya bangi pamoja na vifaa vya kutumia kuvutia ambavyo alikamatwa navyo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere mnamo mwaka jana akiwa anaelekea mkoani.
Haya ndo maneno alioandika Edwin baada ya mkasa huo.
"Kijana wenu nimepatwa na matatizo usiku wa kuamkia Leo
Msanii Chid Benz kanipiga bila sababu akidai eti nilimpiga Picha kipindi yuko Mahakamani akisomewa shtaka lake na kuzipost Hapa Eti Jamani Ngoja niwaulize Mimi niliwahi kupost Picha za Mahakamani Hapa?, na kwanza hiyo tarehe aliyonitajia kuwa niliyompiga Picha nilikuwa niko Zangu Afrika Kusini daaaaahh kiukweli umenikeraa sana kitendo cha kunipiga ngumi na kunikunja T shirt yangu Kama mwizi na kunipa mkwara usio wa maana wowote ila powaaa Mungu ndio mlipaaa wa yoteee Chid Benz........ Mimi bado kijana natafuta riziki brooo na sio niliyekupiga picha...."
0 comments :
Post a Comment