HATIMAYE Msanii wa muziki nchini Ally Kiba ‘Alikiba’ amewajibu baadhi ya wapenzi wa muziki waliokosoa video ya wimbo wake wa ‘Mwana’ au Mwana Dar es Salaam wanaodai kuwa haiendani na kile kilichoimbwa.
Alikiba alisema alichokifanya alimaanisha hivyo kuleta picha mpya kwenye vichwa vya watu.
“Utofauti wa video ndio uzuri wake kwa sababau kila mtu kwenye akili yake amejenga video, amejiwekea wazo kuwa video itakuwa vipi,” alisema
Alisema kwa sababu wimbo umeelezea vitu vingi ni pana, ina vitu vingi kama madawa, ukahaba, ubakaji, wizi, hivyo kutokana na vitu hivyo asingeweza kuweka vyote kwenye video hiyo kutokana na kila mtu ana upeo wake wa kufikiri.
“Nimefanya tofauti kwenye hii video ambapo nilijihusisha sana kwenye kucheza na kuonesha hisia za kuimba zaidi, video nyingi zimeshafanyika hivyo duniani sio ya kwangu tu, hivyo watu wasishangae vitendo havikuwepo nimemaanisha sio nimefanya tu ili nitoe video,” alisema.
Alikiba alitoa ufafanuzi huo wakati akihojiwa na Radio Clouds Fm kwenye kipindi cha 255 ya xxl, aliongeza kuwa utofauti uliopo ndio uzuri wa video, wataalamu walifanya hivyo kwa sababu imetengenezwa vizuri hivyo wakashauriana na kukubaliana waifanye iwe hivyo.
0 comments :
Post a Comment