.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

Kicheko cha Wema na Aunt Ezekiel Kwenye Kaburi la Ngwea Chawashangaza Wengi!

Kicheko cha Wema na Aunt Ezekiel Kwenye Kaburi la Ngwea Chawashangaza Wengi!
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, waigizaji Wema Sepetu na rafiki yake Aunt Ezekiel wameonekana wa kiangua kicheko na kutuma mesegi kwa simu wakiwa juu ya kaburi  la aliekuwa msanii wa Bongo Fleva, marehemu Albert Mangweha ‘Ngwea’.
Kwa mujibu wa GPL,tukio hilo lilitokea Januari Mosi, mwaka huu ambapo Wema akiwa na team yake nzima ya Endless Fame walitembea kaburini hapo yaliyopo Kihonda mjini Morogoro wakiwa wakitokea Dodoma kuja Dar.
Inaelezwa kwamba awali inadaiwa kuwa walipanga mara  baada ya kufika kwenye kaburi hilo wangefanya dua fupi kwa ajili ya kumwombea marehemu apumzike kwa amani huko aliko.Lakini cha ajabu, kabla ya ibada hiyo, Wema, Aunt na wafuasi wao walikuwa wakipiga stori za hapa na pale na katika hali ya kushangaza zaidi, ilifika mahali wakaanza kucheka kile kicheko cha kuvunjika mbavu bila shuhuda wa tukio hili kujua nini hasa kilichokuwa kikiwachekesha!
Kitendo hichokomewashangaza wengi japokuwa Wema akizungumzia tukio hili alisema;
“Tumepita hapa ili kumuombea ndugu na rafiki yetu Mangwea hivyo hatuna lengo lingine zaidi ya hilo.“Ishu ya kupiga stori na kucheka, tusingeweza kuacha kuongea eti kisa tupo kaburini, maana kila kitu lazima kijadiliwe hata kukaa hapa tumekaa kwa sababu tunafarijika kuona kaburi la mwenzetu.”-Wema
Sidhani kama walipanga kufanya hivi,bali naamini walikuwa na nia njema na udaku ndio uka-take advantage.
Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad