*Aungana na timu Zanzibar leo *Phiri afungasha virago
Asha Kigundula
KOCHA mpya wa Simba, Goran Kapunovic ‘Kapu’ tayari ametua Dar es Salaam
akitokea Serbia na kusema kuwa amefurahia ujio wake Tanzania na kuitumikia klabu
kubwa.
Asha Kigundula
KOCHA mpya wa Simba, Goran Kapunovic ‘Kapu’ tayari ametua Dar es Salaam
akitokea Serbia na kusema kuwa amefurahia ujio wake Tanzania na kuitumikia klabu
kubwa.
Akizungumza mara baada ya kuwasili, kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaan jana, Kapunovic alisema amefurahi kupata
nafasi ya kuja nchini na kuifundisha klabu kubwa kama ya Simba ambayo inafahamika katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
nafasi ya kuja nchini na kuifundisha klabu kubwa kama ya Simba ambayo inafahamika katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Alisema ni mara yake ya kwanza kuja nchini, hivyo hawezi kuzungumza mengi kwa sababu bado hajakaa na kuzungumzia mkataba wake wa kuifundisha klabu hiyo.
“Nashukuru sana kupata nafasi ya kuja Tanzania na kuifundisha Klabu ya Simba, ila siwezi kuzungumza mengi mpaka nitakapokamilisha mazungumzo na kusaini mkataba wa kuinoa Simba,” alisema Kapunovic.
Kocha huyo anatarajia kusaini mkataba wa mwaka mmoja leo
jioni kwa ajili ya kuinoa timu hiyo.
jioni kwa ajili ya kuinoa timu hiyo.
Kapu amewahi kuinoa timu ya Polisi Rwanda, Dong Tam Long An ya Vietnam aliyowahi kuichezea mshambuliaji wa zamani wa Simba ambaye anaichezea Yanga kwa sasa, Danny Mrwanda.
Ujio wa kocha huyo, umefungua milango ya kuondoka aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Patrick Phiri ambaye juzi usiku alivunjiwa mkataba wake.
Phiri alitarajiwa kuondoka jana usiku, ambapo tayari uongozi wa Simba umeshamalizana naye kwa kumlipa fedha zake alizokuwa anadai.
Wakati huo huo kikosi cha timu ya Simba kimeondoka Dar es
Salaam, jana kwenda visiwani Zanzibar, katika michuano ya kuwania Kombe la
Mapinduzi.
Salaam, jana kwenda visiwani Zanzibar, katika michuano ya kuwania Kombe la
Mapinduzi.
Kikosi hicho kimeondoka bila ya nyota wake saba, wanne wakiwa ni wachezaji wake wa kigeni kutoka Uganda ambao wametoa sababu mbalimbali.
Miongoni mwa nyota hao ni Simon Sserunkuma na Juuko Murshid ambao wamegoma kuingia kambini kwa sababu ya kudai fedha zao za usajili zilizobaki, huku Joseph Owino, akidaiwa kuumia, hata hivyo Jambo Leo lina taarifa za uhakika kuwa nahodha huyo ana matatizo na viongozi.
Mshambuliaji Emmanuel Okwi, ana matatizo ya kifamilia nchini
Uganda, wakati Jonas Mkude anauguliwa na baba yake, Shaban Kisiga naye ana matatizo ya kifamilia huku Ivo Mapunda akiwa ameruhusiwa kwenda Mbeya kwenye arobaini ya mama yake mzazi.
Uganda, wakati Jonas Mkude anauguliwa na baba yake, Shaban Kisiga naye ana matatizo ya kifamilia huku Ivo Mapunda akiwa ameruhusiwa kwenda Mbeya kwenye arobaini ya mama yake mzazi.
Kikosi hicho kimeondoka chini ya kocha msaidizi Seleman Matola, ambaye atakaimu nafasi ya kocha mkuu mpaka atapoanza kazi kocha huyo mpya.
Wakati huohuo, kikosi hicho cha Simba leo kinashuka kwenye
Uwanja wa Amaan kuvaana na Mtibwa Sugar.
Uwanja wa Amaan kuvaana na Mtibwa Sugar.
Mechi hiyo itaanza majira ya saa 2 usiku ikitanguliwa na mchezo kati ya
ya JKU na Mafunzo ambazo zitaanza saa 10 alasiri, timu hizo
zinazocheza leo ni za kundi (B).
ya JKU na Mafunzo ambazo zitaanza saa 10 alasiri, timu hizo
zinazocheza leo ni za kundi (B).
0 comments :
Post a Comment