.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

Mtuhumiwa apigwa risasi akitoroka Kisutu, Akutwa na ramani ya mahakama ya Kisutu STORI NZIMA IPO HAPA

*Mtuhumiwa apigwa risasi akitoroka Kisutu
*Akutwa na ramani ya mahakama ya Kisutu
*Mbinu za kijeshi zatumika kabla ya kumpiga
Na Grace Gurisha
TUKIO la askari wa Jeshi la Magereza nchini kumpiga risasi mtuhumiwa wa dawa za kulevya akiwa chini ya ulinzi ambaye alikuwa anataka kutoka Mahakama ya Kisutu Dar es Salaam, limekuwa kama filamu ambayo imefunga mwaka 2014 na kuukaribisha mwaka 2015.
Mtuhumiwa huyo aliyepigwa risasi amefahamika kwa jina la Abdul Koroma (33), ambaye ni Raia wa Sierra Leone, alipigwa risasi jana asubuhi katika eneo hilo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam.
Ilikuwa hivi
Saa mbili asubuhi jana, gari ya kubeba mahabusu iliwasili katika mahakama hiyo ikiwa na mahabusu mbalimbali, akiwemo Koroma.
Baada ya kufika mahabusu wote walishuka na kuingizwa mahabusu iliyopo mahakamani hapo, wakati wanasubiri kuanza kwa kesi zao.
Wakati wakisubiri kuingia mahakamani Koroma aliomba kwenda chooni, ambapo aliongozwa na moja ya askari magereza waliokuwa eneo hilo.
Nini kilifuata?
Wakati Koroma akiwa chooni alivua suruali yake aina jinsi na kubaki na bukta, ambapo alivaa suruali hiyo mikononi ili aweze kupenya kwenye uwazi wa juu ya choo hicho kwa sababu kulikuwa na vioo ambavyo vilikuwa vimechomekwa kwa lengo la ulinzi.
Koroma alifanikiwa kwa mbinu hiyo kwa kupenya na kuangukia nje ya choo hicho, ambacho kinatumiwa na mahabusu tu.
Kitendo hicho kilisababisha kukatwa na vioo, hivyo mikononi ilhali alikuwa amevaa suruali yake mikononi.
Askari washtuka
Baada ya mtuhumiwa huyo kuruka ndipo askari waliokuwepo katika eneo hilo walianza kumfukuza, huku wakiwa wamebeba silaha za moto.
Wakati akikimbia alikutana na wanawake wawili, ambapo aliwakamata kwa muda kidogo ili asipigwe risasi, mbinu ambayo iliwafanya askari washindwe kufyatua risasi kwa muda huo.
Awasukuma wanawake
Koroma baada ya muda aliwasukuma wanawake hao na kuendelea kukimbia, alikutana na mlinzi mmoja wa mahakama hiyo ambaye alijulikana kwa jina la Mwakasisi na kumuuliza wewe vipi?
Kwenye akili yake alikuwa akiwaza kuwa ni mwizi, kwa hiyo alitaka kumkamata, ambapo Koroma aliendelea kukimbia.
IMG-20141231-WA0044
Sauti za askari
Wakati watu waliokuwa eneo hilo wakitafakari kinachoendelea, sauti za askari zilianza kusikika wakisema ‘jamani walinzi fungeni geti’.
Kipindi hicho askari walikuwa wamefika getini, hali iliyomfanya raia huyo wa Sierra Leone kubadilisha uelekeo wake wa kutoka getini na kuelekea kwenye ukuta wa mahakama.
Kama kawaida ya maeneo mengi ya mahakama, ukuta wa Mahakama ya Kisutu licha ya kuwa, mrefu lakini juu yake umewekewa nondo ambazo zimechongoka, ambapo mtu akitaka kupita lazima atanasa.
Ikawaje?
Wakati Koroma akiendelea na harakati za kutaka kutoroka licha ya ulinzi mkali wa askari, sauti ziliendelea kusikika.
Kwa sehemu kubwa sauti hizo za askari zilikuwa za wale wenye vyeo vikubwa waliokuwa wakitoa maelekezo kwa askari wadogo waliokuwa na silaha za moto.
Sauti hizo zilikuwa zikitoa maelekezo ya kutaka askari waliokuwa na silaha wasifyatue risasi kwa sababu wataua raia ambao hawana hatia.
Watakiwa kusubiri
Pamoja yote hayo ya kuhakikisha mtuhumiwa huyo hachomoki eneo hilo la mahakama, askari waliokuwa na silaha walitakiwa kusubiri mpaka afike sehemu nzuri na kauli hizo walizitoa baada ya askari hao kuwaambia wakubwa wao kuwa, wanafyatua risasi.
Risasi hewani
Hali hiyo ilimfanya askari mmoja afyatue risasi mbili hewani ili mtuhumiwa aweze kujisalimisha, lakini alikaidi amri hiyo na kuendelea kuparamia ukuta wenye nondo.
Wakati akiruka, fulana yake iling’ang’ania kwenye nondo, huku mguu wake ukiwa umeshikiliwa na mlinzi Mwakasisi, ndipo mtuhumiwa huyo alipopigwa risasi na askari magereza.
Mbinu za kijeshi
IMG-20141231-WA0047
Kwa kweli askari magereza aliweza kutumia mbinu ya kijeshi na kuweza kufyatua risasi ambayo ilimchubua mtuhumiwa kwapani na kupitiliza kichwani ambapo pia ilimchubua bila risasi hiyo kumjeruhi Mwakasisi na watu waliokuwepo eneo hilo.
Apigwa risasi
Katika hali ambayo haikuwa imetarajiwa na wengi, ikabainika tayari mtuhumiwa huyo alipigwa risasi ya kichwani na damu zikawa zinavuja.
Kwa walioshuhudia tukio hilo walichoona wao ni damu tu ikimwagika kwenye eneo la ukuta alilokuwa amekwama mtuhumiwa.
Gari zaingia
Baada ya mtuhumiwa kupigwa risasi na mwili ukiwa umekwama kwenye nondo za ukuta gari tatu za Jeshi la Polisi ziliwasili eneo hilo na moja likiwa na kitanda cha kubebea wagonjwa (machela).
Askari watatu walipanda juu na kumnasua Koroma alipokuwa amenasa kwenye nondo, huku akiwa anavuja damu.
Sauti zaendelea
Sauti ziliendelea kusikika kutoka kwa askari wengine wakisema jamani ongezeni glovu kwa sababu mtuhumiwa anatoa damu nyingi.
Mtuhumiwa huyo aliwekwa kwenye machela na kuingizwa katika gari moja ya polisi na kupelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Akutwa na ramani ya Kisutu
Askari waliokuwa eneo hilo baada ya kumpekuwa mtuhumiwa huyo, alikutwa na ramani ya eneo la Mahakama ya Kisutu, namba za simu za watu ambao wanadaiwa kuwa, walikuwa wakimsubiri kwa ajili ya kumpokea atakapotoroka.
Noah yashikiliwa
Katika sakata hilo inasemekana kuwa, kuna gari aina ya Noah rangi nyeupe imeshikiliwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya uchunguzi.
Kutokana na taarifa kuwa, gari hilo lilikaa muda mrefu nje ya mahakama hiyo, jambo ambalo liliwashangaa watu wa eneo hilo kwa sababu wamezoea kuona teksi zinazoegesha eneo la nje ya ukuta wa mahakama.
Ilielezwa kuwa, gari hiyo ilikuwa imeegesha upande wa pili wa teksi, ambapo ilikaa muda mrefu hali iliyotia mashaka makubwa na wananchi waliokuwa eneo hilo kuhisi gari hilo lilikuwa likimsubiri mtuhumiwa.
Ndani ya gereza la Keko
Askari Magereza (jina tunalo), alisema mtuhumiwa huyo muda mwingi alikuwa akifanya mazoezi na pia alikuwa mkorofi kwa kuwapiga wenzake.
Askari huyo aliendelea kusema kuwa, mtuhumiwa alivyokuwa gerezani hakuwahi kujaribu kutoroka, lakini tatizo lake lilikuwa nikuonea wenzake kwa kuwapiga.
Mashtaka
Koroma alikuwa akikabiliwa na shtaka la kuingiza dawa za kulevya nchini aina ya Cocaine gramu 1229 zenye thamani ya sh. milioni 61.4, Desemba 2, 2013 alikamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akiwa na dawa hizo.
Kesi hiyo namba PI 21/2013 ilikuwa mbele ya Hakimu Mkazi, Augustina Mmbando wa mahakama hiyo, ambapo Mmbando alibadilishwa na kupewa kesi hiyo Hakimu mwingine ambaye ni Warialwande Lema ambaye ndiye anayesikiliza kesi hiyo.
Kesi hiyo ilikuja jana katika mahakama hiyo kwa kutajwa. Wakili wa Serikali Leornad Challo aliieleza Mahakama kuwa, wanasubiri hati itakayothibitisha kifo cha Koroma ili waweze kufunga mashtaka dhidi yake kama sheria inavyoelekeza.
Mpaka mtuhumiwa huyo anataka kutoroka, upelelezi wa kesi dhidi yake ulikuwa bado haujakamilishwa na upande wa mashtaka.
Wakati huo huo, Mwendesha Mashtaka Mkuu wa mahakama hiyo, Tumaini Kweka alisema Koroma alikuwa akituhumiwa kwa shtaka la dawa za kulevya na alitaka kutoroka, ndipo akapigwa risasi.
“Hili ni tukio la mara ya pili watuhumiwa kutaka kutoroka katika mahakama hii,” alisema Kweka.
Gumzo baada ya tukio
Katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam na mitandao ya kijamii, habari za tukio hilo zilianza kuenea kama upepo wa mvua za masika.
Baadhi ya wananchi walizungumzia tukio hilowalisema, ni kama filamu ya kufungia mwaka wa 2014, hasa kwa kuzingatia ni nadra kusikia kuna mahabusu amepigwa risasi kwa sababu ya kutaka kutoroka.
Source: Gazeti La JamboLeo
Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad