.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

Raisi wa Sudani Kusini akimbizwa hospitalini

Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir amekimbizwa hospitalini hapo Jana katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, baada ya kuwa mgonjwa, afisa ameiambia BBC.

Mr Kiir anasumbuliwa na matatizo ya kutoka damu puani, alisema afisa huyo. Maelezo zaidi ya hali yake hazipatikani.

Imebidi mkutano wa  viongozi wa kanda kusogezwa mbele, waliitwa ili  kujadili mgogoro wa Sudan Kusini, alisema afisa huyo.

Mr Kiir, 63, ameiongoza nchi tangu uhuru wake kutoka Sudan mwaka 2011.

Mr Kiir aliongoza mazungumzo mjini Addis Ababa Jumatano na kiongozi wa waasi, Riek Machar ili kukomesha vita vya wenyewe kwa wenyewe ambayo vimeua maelfu ya watu tangu Desemba 2013.
Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad