Aliekua kipa namba moja wa klanbu ya Barcelona kwa miaka 14, Victor Valdes leo amesaini mkataba wa miezi 18 katika klabu ya Manchester United inayoshiriki Ligi kuu Uingereza, Valdes ambae alimaliza mkataba na Barcelona na kufanya uamuzi wa kuicha klabu hio ya Hispania na kisha kujiunga na Manchester United rasmi leo Ijumaa 9/1/2015 na kupewa jezi namba 32, huku akitarajiwa kutumika kama kipa namba mbili baada ya David De gea ambae ndo kipa namba moja wa klabu hio.
Leo ijumaa, Valdes amejiunga na kikosi katika mazoezi ambayo ndo mazoezi yake yakwanza tangu alipotia saini asubuhi japo alikua akifanya mazoezi na Manchester United tangu mwezi wa kumi.
Valdes aliweza kuisaidia Barcelona kubeba makombe ya Ligi kuu Hispania mara 6, na makombe ya ligi ya mabingwa ulaya mara 3
0 comments :
Post a Comment