.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

Kajala Masanja Mwigizaji asiyependa maisha ya matanuzi


Kajala Masanja

Na Charity James
KATIKA maisha wengi hupitia mengi yanayofanya mtu kuwa na uwezo mkubwa wa kukata tamaa katika mipango ya maisha ya baadaye.

Kwa kumwongelea msanii nyota wa filamu anayefanya vizuri na kazi yake ya Pishu, Kajala Masanja unaweza kumweka kama mfano mkubwa wa kuigwa kwasababu ameshafanikiwa kupitia changamoto mbalimbali na bado hajaweza kukata tamaa na kuendelea kupambana.

Kajala ambaye ameshapitia changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuhukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela au faini ya sh. milioni 13 amekuja upya na kubadili jina ambapo anajiita New Kajala.

Pamoja na kuandamwa na misukosuko iliyosababisha hata kuwekwa mahabusu kwa muda mrefu, lakini amerudi uraiani akiendelea na kazi zake za uigizaji na ujasiriamali.


Baada ya kutoka mahabusu Kajala ambaye ameamua kubadili jina na kujiita New Kajala anabainisha kuwa sasa sio Kajala aliyejulikana na kila mtu, sasa amekuwa mpya baada ya kujifunza vitu vingi akiwa gerezani.

Anasema kwa vitu alivyopitia amezidi kuwa na nguvu na mvumilivu kwahiyo wanaodhani wanafanya vitu kwa kunikomoa wanajidanganya kwasababu wananifanya niendelee kuwa mtu mwenye nguvu na mwenye kujiamini zaidi.

Anasema matatizo aliyoyapata ilichangiwa na kurukia vitu ambavyo havijui, sasa hawezi kurudia tena hata adanganywe vipi, sasa hawezi kukurupuka tena ameshajifunza.

Kajala anasema bado ana mawasiliano na mwanaume aliyemfanya aweze kuonja  maisha ya gerezani alipokuwa mahabusu, akipata muda huwa anakwenda kumuona lakini hategemei kurudiana naye tena itabaki tu kama alishawahi kuolewa naye kanisani.

"Huwa nikienda kumuona ananambia anapenda kuniona nisimuache anajisikia raha anavyoniona, nikienda kumwona huwa najisikia vibaya, naumia kwa kuwa nazijua tabu anazozipata akiwa ndani," anasema.

Kajala anasema anafikiria kwenda kumtoa lakini uwezo huo hana kwasababu fedha alizoamriwa  sh. milioni 100 hawezi kupata na bado anakesi nyingine nyingi anaendelea kusomewa hivyo hajui hukumu yake ni ipi.

Akizungumzia suala la kazi mara baada ya kurudi uraiani anasema hadi sasa ana filamu tatu ambazo ni pamoja na  ‘Laana’, ‘Pishu’ na ‘Mbwa mwitu’ alizozindua hivi karibuni.

"Nina filamu zangu tatu hadi sasa ambazo nimefanya mwenyewe lakini Laana ni filamu ambayo naiona nzuri kuliko kazi zangu zote," anasema.


Akizungumzia stori inayohusu filamu hiyo, Kajala anasema filamu hiyo ameifanya kama mke wa mtu ambaye ni Gabo halafu anaingia katika ugomvi na mama mkwe wake baada ya kugundua naye anatoka na mwanaye.

Anasema mume wake ambaye ni Gabo anatembea na mama yake mzazi kwaajili ya kupata mali na mama mtu anaanza kumpenda kiukweli mwanaye na baada ya hapo anashindwa kuonesha mapenzi yake kwa muwe wake kwasababu anampenda kiukweli mwanaye.

Pia anasema filamu ya ‘Laana’ ndiyo bora kwake na ilimgharimu fedha nyingi. Ni kiasi cha sh. milioni 12 hadi ilipokamilika, pia hadithi iliyomo ndani ni ya kuvutia zaidi. 
"Unajua siyo jambo la kawaida kwa mama kutembea na mtoto wake," anasema.

Anasema ameamua kufanya hivyo kwaajili ya kutoa elimu kupitia sanaa hiyo kwa kuwataka vijana kuepukana na kitu kama hicho kwasababu nikinyume na maadili. 

Nyota wake
Akizungumzia msanii anayetamani kufanya naye kazi baada ya kurudi upya katika tasnia hiyo Kajala anasema anatamani kufanya kazi na Ndumbagwe Misayo maarufu Thea  kwasababu anajua na anaweza.

Kwa upande wa kiume anasema ameshawahi kufanya kazi na wasanii wengi wa kiume na katika tasnia hiyo anawakubali wasanii wote lakini Kanumba ni msanii ambaye alikuwa anamkubali na alikuwa akitumia muda wake mwingi kumwangalia.





Akizungumzia msanii aliyemshawishi kuingia katika tasnia ya filamu ambayo alikuwa anasitasita kuingia ni Jacob Stephen 'JB' baada ya kumuaminisha kuwa anakipaji na anaweza kuigiza.

Kuhusiana na suala la wasanii kuingia katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya Kajala anasema anaamini huko ndio kuna maslahi zaidi ndio maana wanaamua kuingia huko lakini kwa upande wake haamini kitu kama hicho na hawezi kujikita katika tasnia hiyo.

"Mmmh nitaimba nini mimi siwezi kuimba na sina sauti ya kuimba nitaendelea kukomaa upande huu huu naamini nitafanikiwa kufikia malengo muziki siuwezi," anasema.

Katika hatua nyingine nyota huyo alizungumzia suala la kutembea na mume wa mtu anasema alishawahi kufanya hivyo lakini ni zamani na alijikuta anafanya hivyo bila kujua.

"Wanaume wanaujanja mwingi wanatumia, anaweza akakufuata akakudanganya na wewe unaweza ukajikuta umeshaingia katika tukio hilo, ndio nimeshawahi kutembea na mume wa mtu lakini ni zamani sana," anasema.

Kuhusu Wema

Anasema huwa akikaa mwenyewe nyumbani anamkumbuka kutokana na mambo mengi waliyoyafanya anatabasamu na anaendelea na mambo mengine.

"Siwezi kusema sitaki kumwona utakuwa ni uongo nitakuwa naidanganya nafsi yangu mimi namkumbuka na haya ni maisha tu yapo na yataendelea kuwepo," anasema.

Anasema watu wanaoandika na kuzusha vitu kuhusiana na wawili hao waache kwasababu ndio wanaofanya ugomvi uendelee na kuleta matatizo ambayo hayajengi.



"Tatoo ya Wema siwezi kuifuta nilifanya kwa mapenzi yote na nilifanya kutokana na mapenzi aliyoyaonesha kwangu hivyo sitaifuta hadi nitakapokufa," anasema.


Siri ya mafanikio

Kajala anasema mbali sanaa anajihusisha na uuzaji wa nywele, ana kampuni yake binafsi, kitu kinachofanya kutoa kazi anavyojisikia.

Pia anabainisha kuwa anajua anachokifanya na anajua ndicho kinachomwingizia fedha kwaajili ya mahitaji yake mbalimbali, anaipenda kazi yake na anafanya kwa bidii ili iweze kumwingizia kile anachokitaka.

"Sio ukipata fedha uzitumie lazima uwe na bajeti nazo hii ni kwaajili ya ada kama una mtoto au ni ya kula na familia yako na sio kuzitumia zote ovyoovyo huwezi kuendelea na kufikia malengo," anasema.

Anasema meneja wake anamsaidia sana katika kutumia vizuri fedha zake wakati mwingine akitaka  kutoka humzuia kwa kumweleza kuwa hakuna sababu kutumia fedha ovyo, ni bora hiyo fedha hizo akaifanyia vitu vya maana.

Anasema kwa sasa  yeyesio mtu wa kutoka kwa ajili ya matanuzi, kwa sasa akitoka anakuwa amealikwa na anajua anachofuata anaenda anarudi.

"Zamani nilikuwa natoka sana kila mwishoni mwa wiki hivyo sio kitu kizuri kutoka bila mipangilio namshukuru sana meneja wangu ananifanya nifanye vitu vya maendeleo," anasema.

Kajala amewataka wasichana kama yeye kuacha kuwa na imani za kuamini kuwa hawawezi kufanya chochote bila mwanaume wanatakiwa kujituma watumie fedha yao wasitegemee wanaume fedha ya mtu inauma.

Kuhusiana na Tatoo

Anasema amechorwa tatoo saba mwilini mwake na hajui zina maana gani, aliona watu wanachorwa naye alitamani kuchorwa kwa kuamini kuwa atapendeza. 
"Natamani kuzifuta ningekuwa na uwezo ningefuta zote kwasababu maisha yamebadilika maisha ya zamani na sasa ni tofauti kwasababu naendelea kukua na tatoo, nazeeka nisingependa kuwa hivyo," anasema.

Anasema tatoo alizonazo ni ya Wema, Mtoto wake Paula, Msalaba, Ua na nyingine nyingi ambazo hakutaka kuziweka wazi kuwa zimechorwaje na sehemu gani.
Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad