.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

Simba, Messi kitimoto TFF


 
Asha Kigundula

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeamua kuwaweka kiti moto kati ya uongozi wa klabu ya Simba na mchezaji wao Ramadhan Singano Messi’ kutokana na  tofauti zao kuhusu mkataba kati yao.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TFF kupitia kwa Ofisa Uhusiano wake, Baraka Kizuguto kikao hicho kitafanyika Jumanne (kesho), huku klabu ya Simba na Messi, kila mmoja akitakiwa kupeleka kielelezo chake.

Kikao hicho kimeitwa baada ya Messi akiwakilishwa na Chama cha Wachezaji wa Soka Tanzania (Sputanza) kuomba suluhu kuhusu tofauti ya mkataba, ambapo yeye anao unaoisha Julai mwaka huu, na Simba Julai mwakani.

 

Tayari klabu hiyo pamoja na mchezaji huyo wamepelekewa taarifa za kuitwa katika kikao maalum cha kuhakikisha suala hilo lina malizika.

Simba na Messi, wametofautiana kuhusiana na kila mmoja akidai mkataba wake ndiyo halali huku Simba ikionesha ina mkataba unaoonesha mchezaji huyo amebakiza mwaka mmoja na yeye akidai ameshamaliza mkataba wake wa kuitumikia klabu hiyo.

 Katika taarifa yake, TFF imesema imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za mgogoro wa kimkataba kati ya pande hizo mbili.

"TFF imeagiza mwakilishi wa klabu ya Simba pamoja na mchezaji wa Simba wafike ofisi za TFF siku ya Jumanne tarehe 09/06/2015 kwa mazungumzo," imesema sehemu ya taarifa hiyo.


 Katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye mazungumzo,TFF imeziasa pande zote mbili zijiepushe na kutoa matamko yanayoweza kuchochea hali ya kutoelewana na kuamsha hisia mbaya katika familia ya mpira wa Miguu Tanzania.

Awali Simba, ilisema kuwa inataka kumshtaki mchezaji huyo pamoja na vyombo vya habari ambavyo vimeonekana kulifuatilia suala hilo, ikieleza kuwa habari hizo zinaichafua.

mwisho
Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad