.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

MAREKANI YAMBARIKI NKURUNZIZA AWANIE URAIS


BUNGE la Marekani limeridhia Rais wa Burundi, Piere Nkurunziza, kuwania kiti hicho kwa mara ya tatu nchini humo. Wajumbe wa Bunge hilo wamesema wameguswa na machafuko yanayoendelea nchini Burundi na wameshauri Serikali na raia wa Burundi kumaliza tofauti zao haraka.


Wameshauri pande hizo mbili kushirikiana kwa pamoja ili kuendeleza nchi yao na kufanikiwa kufanya uchaguzi wa huru na wa haki wa wabunge na rais unaotarajiwa kufanyika mwezi huu nchini Burundi.


"Tunaelewa watu wengi wanapinga hatua ya Rais Nkurunziza kutaka kuwania urais kwa mara ya tatu, lakini tunaheshimu pia uamuzi wa mahakama ya kikatiba ya Burundi ambayo imemruhusu kugombea kwa mara nyingine tena," lilielezata tamko hilo.



Baraza hilo limeziomba Jumuiya za Kimataifa kuunga mkono uamuzi huo uliotolewa na Mahakama ya Burundi ili kurudisha amani nchini Burundi. 
Hata hivo wajumbe wa baraza hilo wamesema kuwa wataendelea kuiunga mkono Burundi na kusimama pamoja na raia wa Burundi ili kuwezesha kupatikana kwa amani na maendeleo ya taifa hilo kidemokrasia.


Pia serikali ya Burundi imetakiwa kuhakikisha kwamba uchaguzi utakaofanyika unakuwa uchaguzi wa uhuru na wa haki.
Baraza hilo limesema lina matumaini kwamba Serikali ya nchi hiyo itahakikisha  vyama vya upinzani vinashiriki kikamilifu katika uchaguzi ujao.


Baraza hilo limeongeza kuwa Serikali ya Burundi itoe fursa kwa watu watakaofuatilia uchaguzi huo kimataifa.

Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad