RIO DE JENEIRO, Brazil
MLINZI wa Brazil, David Luiz amefurahishwa kuona timu yake ya taifa imepata ushindi wa kwanza ikiwa nyumbani baada ya kuisha michuano ya Kombe la Dunia mwaka jana.
Brazil iliifunga Mexico mabao 2-0 katika Uwanja wa Allianz Park , Sao Paulo. Magoli ya Brazil yalifungwa na Philippe Coutinho (Dakika 28) na Diego Tardelli (Dakika ya 37).
Mchezaji huyo wa Paris Saint-Germain alisema kuwa , alikuwa na mashaka kuhusu kurejea nyumbani, baada ya Brazi kufungwa mabao 7-1 dhidi ya Ujerumani katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Dunia.
"Kwangu mimi, nilikuwa na mashaka zaidi,"aliiambia Globo.
"Nilikuwa katika hali ya hofu kuhusu kurejea hapa na kucheza dhidi ya Brazil. Mpira wa miguu unatupatia sisi nafasi hii na tukaweza.
"Ni kitu kizuri kucheza nyumbani na kufanya vizuri, kumiliki mchezo kama tulivyofanya. Ninafuraha kumiliki mchezo kama tulivyofanya. Ninafuraha sana kuhusu hilo."
Ushindi wa Brazil ulikuwa wa tisa mfululizo tangu kocha Dunga kuichukua timu kutoka kwa Luiz Felipe Scolari muda mfupi baada ya kuicha michuano ya Kombe la Dunia.
0 comments :
Post a Comment