.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

Samatta: Nitacheza Tanzania baada ya miaka 20





Na Charity James
MCHEZAJI tegemeo wa Taifa Stars, Mbwana Samatta, amesema atarejea nchini na kuichezea moja ya klabu za Tanzania baada ya miaka 20 ijayo.

Samatta kwa sasa ana umri wa miaka 23.

Akizungumza Dar es Salaam juzi, Samatta alisema hana mpango wa kucheza katika klabu za Tanzania kwa sasa hadi pale atakapotimiza ndoto zake.

Alisema baada ya miaka hiyo 20, atakuwa ameshatengeneza maisha yake, hivyo utakuwa muda mwafaka kwake kurejea nyumbani.



"Baada ya miaka 20 ninaweza kurejea Tanzania na kucheza katika moja ya timu za hapa. Nitacheza hata bure kwa sababu nitakuwa nimeshatengeneza maisha yangu," alisema Samata.


Samata alizaliwa Januari 7, 1992 jijini hapa, hivyo baada ya miaka 20 ijayo atakuwa na umri wa miaka 43, umri ambao ni wazi hatakuwa na uwezo mkubwa wa kusakata kabumbu.

Katika hatua nyingine, Samata ambaye anakipiga katika klabu tajiri Afrika ya Tp Mazembe amesema hana mpango wa kuongeza mkataba katika klabu hiyo, kwa lengo la kupata nafasi ya kutimkia katika klabu nyingine.

Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad