LONDON, Uingereza
KIUNGO mshambuliaji Marco Reus, ameongeza mkataba mwingine katika timu ya Borussia Dortmund hadi mwaka 2019.
Reus, ambaye mkataba wake wa awali ulikuwa na kipengere kilichoandikwa kuwa anaweza kuachiwa kwa euro milioni 25, alikuwa akihusishwa na habari za kutakiwa na timu za Real Madrid na Barcelona.
Mchezaji huyo wa Ujerumani ametangaza kwenye akaunti yake ya Twitter kwa kuandika "Nimefurahi kuwafahamisha kuwa nimeongeza mkataba wangu hadi mwaka 2019. Marco!"
Dortmund, ambayo imekuwa ikishindwa kuzuia wachezaji wenye majina makubwa kubakia kama
Mario Gotze na Robert Lewandowski kwenda Bayern Munich katika miaka ya karibuni, imekuwa ikitarajiwa kumkosa Reus baada ya kuwa na wakati mgumu katika msimu wa Bundesliga ambapo kwa sasa imekuwa ikipambana isishuke daraja.
Kwa upande mwingine, Reus alisema kwenye mtandao wake wa Facebook kwamba ameamua kubakia katika mji aliozaliwa baada ya kuusikiliza moyo wake.
Ninaandika: "Nina matumaini ya kuendelea kuwepo BVB pamoja na mashabiki wetu wa kusisimua
. Moyo wangu umeamua. Acha tuanze. Tunataka kufanikiwa mambo mengi. Siyo tu msimu huu."
Katika mahojiano na Ruhr Nachrichten, Reus aliongeza: "Niliposaini
Dortmund,nilisema kuwa ninataka kufanikiwa vitu na klabu. Nimekuwa na hisia kwamba haijaisha, hasa ukizingatia hali yetu ni ngumu kwa sasa."
Katika mkataba wake wa sasa hakuna kifungu kinachoruhusu kuvunja mkataba kama ilivyokuwa mwanzo euro milioni 25 .
Awali ilikuwa ikielezwa kuwa klabu za Chelsea na Manchester City za Uingereza ambapo Mkurugenzi wa michezo wa BVB amethibitisha kuwa Marco Reus angeweza kujiunga na moja ya klabu kubwa duniani, lakini mwenyewe ameamua kubakia.
0 comments :
Post a Comment