.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

Steve Mengele autaka Ubunge wa Kinondoni




MSANII wa filamu nchini Steven Mengere 'Steve Nyerere' amewataka watanzania wenzake kujitokeza kuandikisha katika daftari la wapiga kura, ili wasikose kupiga kura katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

Akizungumza katika mkutano maalum wa kutangaza nia na kuhamasisha watu kujiandikisha, alisema kujiandikisha ni haki ya kila Mtanzania hivyo kwa vijana na wazee hakuna sababu ya kukaa na kuacha muda unapita bila ya kuutumia.

Nyerere alisema ni haki kwa kila Mtanzania kwenda kujiandikisha hivyo hakuna sababu ya kuacha kipindi hicho kinapita bila ya wao kukitumia.



"Mama zangu, Baba zangu, Vijana wenzangu, jitokezeni kujiandikisha ni haki yenu ya msingi, hasa katika uchaguzi mkuu ujao"alisema Steve Nyerere.

Pia Nyerere alisema atahakikisha anatatua changamoto za wananchi wa jimbo la Kinondoni pindi atakapopata ridhaa ya kuliongoza jimbo hilo.

Hayo aliyasema juzi wakati akitangaza nia ya kuwania ubunge wa Kinondoni kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.



Msanii huyo alisema wilaya hiyo ina changamoto nyingi ambazo zinapaswa kutatuliwa ili wananchi waweze kuishi maisha ambayo hayana kero.

Alisema huu ni wakati wa mabadiliko na mabadiliko yataletwa na yeye kwa kuwa anazijua changamoto nyingi ambazo zinawakabili wananchi hao.

"Mimi Steve Nyerere nimeamua kwa dhati kujitoa na kutangaza nia ya kuwania ubunge ili nisaidiane na wananchi wa Kinondoni kwa ajili ya kuijenga Kinondoni mpya," alisema Steve.

Alisema Kinondoni inapaswa kuwa ya mfano kwa kuwa na mitaa iliyopangwa katika mpangilio maalumu na mitaro iliyosafishwa vyema.

Alisema licha ya hilo, Kinondoni inapaswa kuboreshwa miundombinu ili kuzuia mafuriko ambayo 

yamekuwa yakitokea mara kwa mara na kuharibu sifa ya jimbo hilo linaloubeba mkoa wa Dar es Salaam.
Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad