Thierry Henry: ARSENAL HAWAITAJI MCHEZAJI MWENYE UJUZI MWINGINE
NYOTA wa zamani wa Arsenal, Thierry Henry amesema washika Bunduki hao hawaitaji mchezaji mwenye ujuzi katika usajili huu wa majira ya Joto kwasababu tayari wanaye Alexis Sanchez.
Alexis amefunga mabao 25 katika msimu wake wa kwanza Ligi Kuu England baada ya usajili wa pauni milioni 35 akitokea Barcelona na kuweza kusaidia washika bunduki kubeba Kombe la FA Mei, 2015.
Arsene Wenger anatarajia kuboresha kikosi dhidi ya ligi ya msimu ujao ila Henry ana amini kiungo huyo wa Chile ameshaonesha maajabu.
"Ndio tunatakiwa kuongeza wachache ila mchezaji maalumutayari ni Alexis Sanchez," Henry aliiambia mtandao wa Goal wakati wa uzinduzi wa jezi za nyumbani za Puma zitakazotumiwa na Arsenal msimu ujao.
"Alexis anahitaji kutulia kidogo. Ameshakuwa na msimu mzuri ila natarajia awe bora zaidi mwakani. Kama ataweza kuepuka majeraha, yeye ndo yule anayeweza kukusaidia kushinda ligi.
"Alexis amekuwa vizuri na Mesut Ozil amekuwa vizuri sana tangu afike, ila moja ya nyakati muhimu kwangu mwaka huu ni jinsi Francis Coquelin ameweza kumudu nafasi ya kiungo, na hakuigharimu Arsenl chochote.
"Mara tu baada ya Francis kuingia kwenye timu, Santi-Cazorla alicheza vizuri zaidi, Alexis Sanchez ni moto, Olivier Giroud anafunga mabao.
"Huwezi kushinda mataji tu kwa sababu wewe unatumia fedha. Unahitaji kuwa na uwiano sawa katika timu na msimamo. Fedha haiwezi kukununulia wewe mataji daima."
Arsenal walipoteza michezo 7 ya ligi msimu ulioisha na wamemalizi wakiwa nafasi ya 3 ila walionesha uwezo wao kwa kushinda mechi nane mfululizo kati ya Febuari hadi Aprili.
Henry amekubali kuwa washika bunduki wanabidi waongeze uthabiti katika wakati huu wa kampeni na pia ana amini wachezaji wanne wanahitajika ili wachukue taji kutoka kwa Chelsea.
"Unahitaji uthabiti ili ushinde ligi," Henry aliongeza. " Kushinda taji, utakiwi kupoteza mechi zaidi ya mbili au tatu. Hicho ndo kinahitajika.
"Kikosi kizuri. Nadhani wachezaji muhimu wanaweza kuongezwa na ni maamuzi ya Arsene kama anataka kufanya.
"Bado nadhani tuna upungufu wa mlinda mlango, mshambuliaji, kiungo wa nyuma na beki mmoja. Kocha Arsene anajua zaidi ya kila kitu nini timu inahitaji ila uthabiti ni muhimu."
Thierry Henry alikuwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa jezi mpya za Arsenal, ambazo zimeanza kuuzwa Juni 25, 2015.
0 comments :
Post a Comment