NYOTA wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ali Kiba 'Alikiba', amejitokeza na kupuuzia mbali madai kwamba alipendelewa katika Tamasha la Tuzo za Muziki Tanzania (KTMA).
Alikiba, ambaye alipata tuzo tano kwenye tamasha hilo na kumshinda mpinzani wake kwenye muziki huo, Diamond Platinum, alisema kamwe hakupendelewa ila muziki wake unapendwa na wengi tofauti na baadhi ya watu wanavyofikiria.
Alitoa kauli hiyo wakati akihojiwa na Televisheni ya Citizen ya Kenya, na kusema kuwa anahisi yeye ndio bora na kwamba ilikuwa haki yake kushinda tuzo hizo kutokana na kujituma kwake.
Sambamba na hilo alisema hana ugomvi na Diamond, na kusema anakerwa na watu wanaomlinganisha na msanii huyo na kudai kuwa yeye ni yeye na Diamond ni Diamond.
0 comments :
Post a Comment