STAA wa muziki wa kizazi kipya, Henry Samili 'Mr Blue', amesema katika maisha yake ya muziki anakumbuka tamasha lake la kwanza kufanya alilipwa sh. 200 kama nauli na msanii mwenzake Dudubaya.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Bluu alisema hakuona kitu cha ajabu kipindi hicho kwasababu alikuwa anafanya muziki ili ashangiliwe akiwa jukwaani.
Alisema furaha yake katika muziki ilikuwa ni kushangiliwa na wapenzi wa kazi zake akiwa jukwaani kitu ambacho kilikuwa kinampa imani ya kuamini anaweza kuimba.
"Nakumbuka na sitokuja kusahau siku hiyo ambayo niliondoka kwa furaha kubwa baada ya mashabiki waliojitokeza katika tamasha hilo kuunga mkono juhudi zangu nilipokuwa ukumbini natumbuiza," alisema.
Alisema alikuwa anaimba muziki kutokana na mapenzi na sio kwaajili ya fedha hivyo kwa sasa imekuwa tofauti kutokana na wasanii kufanya muziki kibiashara zaidi.
0 comments :
Post a Comment