Watu sita (wanawake 4 ikiwa ni pamoja na mama mjamzito) (wanaume 2) wamepoteza maisha papo hapo katika ajali ya gari iliotokea Kaskazini Magharibi mwa Hispania.
Ajali hio imesababishwa na gari ilokuwa spidi na kutoka nje ya barabara ya mashindano. Polisi wamesema majeruhi wapo 16 ikiwa ni pamoja na watoto watatu, baadhi ya majeruhi wameumia vibaya sana baada ya ajali hio katika mashindano ya magari ya Coruna
Matangazo ya Televisheni yalionesha gari ikipoteza muelekeo na kutoka nje ya barabara mpaka kwa mashabiki katika wingu la vumbi. Police wanasema gari ilikuwa mwendo wa haraka sana.
Waziri Mkuu Mariano Rajoy ameonesha rambirambi yake kupitia mtandao wa kijamii wa twitter.
Amesema mashindano hayo yamepatwa na maombolezo
"Rambi rambi zangu za dhati kwa wale waliouawa. Nawaombea majeruhi wote wapone haraka," aliongezea.
Ajali imetokea jioni ya jumamosi karibu na mji wa Carral katika jimbo la Galicia.
Vyombo vya habari chini Hispania vimeripoti kuwa madereva hawakuwa miongoni mwa waliopatwa na majeraha.
Mashndano hayo yamesimamishwa. Zaidi ya watu 140 walikuwa wakishiriki.
0 comments :
Post a Comment