.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

Muro, Manara, acheni sifa


Afisa Habari wa Klabu ya Yanga Jerry Muro


IMEKUWA ni mipasho baada ya kutoa taarifa kwa wadau wa mpira wa miguu, kitu ambacho sidhani ndicho walichoandika katika mikataba wao.

Mipasho kadhaa imekuwa ikitolewa na Maofisa Habari wa klabu mbili kubwa hapa nchini Simba na Yanga, Haji Manara wa Simba na Jerry Muro wa klabu ya Yanga.

Kauli za mipasho zimekuwa zikisikika kila mara kwa maofisa habari hao, ambao kila mmoja akitaka kuonekana bora kwa wanachama wa klabu yake.

Maofisa hao sasa waonekana kama hawatambui wajibu wao kwa kushindwa kufanya kazi zaidi ya kupeana maneno ambayo wazi hayawajengi zaidi ya kuwashusha.

Wasemaji hao walitofautiana katika suala la usajili, lakini baadae ikawa sehemu ya kila mtu kutaja maisha yake binafsi, siamini kama wanajenga zaidi ya kubomoa.


Afisa habari wa klabu ya Simba Haji Manara

Sidhani kama kuna mtu alikuwa akidhani watafanya mambo ya aina hii, tena kila mmoja akimtaja mwenzake na kudhihaki kabila za wenzao kitu ambacho naona sio kizuri.

Haiwezekani utaje kabila na kuidharau, wakati nawe ni mtanzania ambaye una moja ya kabila za Tanzania, siamini kama hakuna sehemu yenye matatizo.

Kauli zao zinaonesha wazi ni kulewa sifa ya madaraka na kushindwa kujua nini wajibu wao kama viongozi wawakilishi wa klabu hizo kubwa Afrika Mashariki.

Kwa kauli zao wanaonesha wazi nafasi hizo zimewashinda, badala ya kufanya wanachotumwa wanajikuta wakileta mipasho kwenye vyombo vya habari.

Hata hivyo sijaona sababu hata baadhi ya radio kuvifurahia vitu hivyo na kutoa sauti zao, kitu ambacho sioni kama kina maana kubwa.

Wajibu wenu ni kuhabarisha wadau wa mpira wa miguu na si kuleta mambo ya mipasho katika vyombo vya habari, sioni kama watu wanawasifia zaidi ya kuwacheka.

Fuateni wajibu wenu na si kuendekeza marumbano, sidhani kama inajenga zaidi ya kubomoa.

Muro, Manara michezo ni furaha na si marumbano achani marumbano, sidhani kama inawasaidia zaidi ya kuwashusa na kuwadharaulisha, sijaona hoja zaidi ya sifa.

Maisha binafsi yamechukua nafasi wakati kazi yenu ni kuzungumzia klabu zenu na sio kujionesha mna maisha bora, hakuna anayetaka maisha yenu zaidi ya kuhabarisha mambo ya klabu zenu.






Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad