.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

Simba SC yaivutia pumzi Mwadui FC Mwanza




Kikosi cha Simba, kimejikita mkoani Mwanza kwa ajili ya kambi maalumu ya kujiandaa na mchezo wa Jumamosi dhidi ya Mwadui Fc.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Ofisa Habari wa klabu hiyo, Haji Manara alisema kikosi chao kinaondoka mkoani Mwanza Alhamisi ikiwa siku mbili kabla ya mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

HAJI MANARA (kulia) MSEMAJI WA SIMBA

Manara alisema kikosi chao kitaendelea kuwepo mkoani humo hadi siku hiyo ambayo itaanza safari ya kwenda mkoani Shinyanga kuvaana na vijana wa Jamhuri Kihwelo 'Julio'.

Simba inaenda Shinyanga kuvaana na Mwadui FC, ikiwa na kumbukumbu ya kutoka sare ya bao 1-1 na Toto Africans ya Mwanza.

Matokeo yaliyopita yamezidi kuitibua Simba ambayo safri yake ya kusaka ubingwa wa mwaka 2015/16 inazidi kufifia kutokana na kufikisha point 23 ikishika nafasi ya nne huku Yanga ambao ndio vinara ikiwa na point 30.

Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad