.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

Maguli akerwa na kipigo cha Yanga



Mshambuliaji wa Stand United anayeongoza kutikisa kamba, Elius Maguli, amesema bado wanaumizwa na kipigo kikali cha mabao 4-0 walichopata kutoka Yanga wikiendi iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa.

Akizungumza jijini Dar es salaam jana, Maguli alisema kuwa mbali na kipigo hicho, lakini pia siku hiyo alicheza chini ya kiwango.

"Naumizwa na mambo mawili, kwanza tumefungwa idadi kubwa sana ya magoli pamoja na kujianda vizuri, lakini pia naona kama sijafanya kitu kuisaidia timu yangu," alisema maguli.



alisema kuwa kiwango kibovu alichokionesha kwenye mchezo, kimemsikitisha ingawa hayakuwa matarajio yake.

"Kwenye soka siyo wakati wote unaweza kuwa kwenye kiwango kizuri, unaweza kucheza vizuri mechi hii, kisha ukafanya vibaya mechi ijayo," alisema Maguli.

Katika mchezo huo maguli alishindwa kufurukuta mbele ya safu ya ulinzi ya Yanga iliyokuwa ikiongozwa na Kelvin Yondani na Vicent Bossou.

Maguli alipiga shuti moja pekee lililolenga goli na kocha Patrick Liewig alimpumzisha zikiwa zimebaki dakika 20.
Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad