.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

Safari za Nje ndo zimenifanya niwe kimya




Baada ya kutamba na wimbo wa 'Wanjera', msanii nyota wa muziki wa kizazi kipya Ommy Dimpoz amezindua video ya wimbo wake mpya wa 'Achia Body' na kueleza ukimya wake wa muda mrefu.

Dimpoz alizindua video hiyo wiki iliyopita na kusema kuwa ukimya wake wa muda mrefu wa bila kutoa nyimbo mpya ulitokana na kutingwa na maonyesho mengi ya nje ya nchi.

'Nilikuwa na shoo nyingi za nje. Lakini hii kazi yangu mpya ni nzuri na watu wataifurahia sana na sasa kuna mambo makubwa sana, sio kwamba nimeshuti na magari makali, nimeshuti na wanajeshi au maghorofa hapana! Hii kazi ni nzuri."

alisema kuwa amezindua video ya wimbo huo kwa sababu anajua amekaa muda mrefu bila kutoa ngoma kwa vile ratiba yake ilikuwa ngumu na sasa anajiweka karibu na wadau wa muziki."

Msanii  huyo pia alisema kuwa anajivunia na kufurahishwa na hatua aliyopiga katika tuzo za kimataifa baada ya kushinda tuzo ya 'Best New Artiste Africa' katika tuzo za afrimma na tuzo za People's Choice Award katika tuzo za African Entertainment Awards USA.

Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad