.

.

SHOP HERE

News
Loading...

.

.

.

shop now

MAYUNGA KUACHIA VIDEO YA 'PLEASE DONT GO AWAY' ALIOFANYA NA AKON


Mshindi wa shindano la Airtel Trace Music Stars Afrika, Nalimi Mayunga akirekodi video yake na mwanamuziki nguli wa miondoko ya R& B Akon nchini Marekani.
mwanamuziki nguli wa miondoko ya R& B Akon akiwa na Mshindi wa shindano la Airtel Trace Music Stars Afrika, Nalimi Mayunga mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa Airtel Trace Music Stars Afrika  mwaka Jana.
*************
MSHINDI wa shindano la Airtel Trace Music Stars Afrika, Nalimi Mayunga anategemea kuzindua video yake  mpya “Please don’t go away” aliyoifanya na mwanamuziki nguli duniani  'Akon' huko nchini Marekani

Nalimi Mayunga alipata nafasi  ya kurekodi wimbo huo  mara baada ya kuibuka kuwa mshindi wa Airtel Trace Music Stars Afrika na kuwashinda washiriki wengi  kutoka  nchi 12 barani Afrika

Kibao hicho chenye mahadhari ya R&B  kimeanza kupigwa au kuchezwa leo katika radio mbalimbali nchini wakati ambapo video yake inategemewa kuzinduliwa rasmi siku ya Ijumaa 20 Mei 2016 wakati wa finali za msimu wa pili wa shindano la Airtel Trace Star 2016 linalowashirikisha washindi watano bora ambao wanashindania kitita cha shilingi milioni 50 ikiwa ni pamoja na nafasi kuiwakilisha Tanzania katika michuano ya AfrikaAirtel Trace Star yatakayofanyika hivi karibuni nchini Nigeria

Akiongea kuhusu wimbo wake na Akon, Mshindi wa shindano la Airtel Trace Music Stars Afrika, Nalimi Mayunga alisema “ kwa kweli namshukuru Mungu sana kwa kuniwezesha kufika mpaka hapa lakini pia nawashukuru Airtel kwa kunipa nafasi hii kubwa ya kuweza kurekodi wimbo na Mwanamuziki wa kimataifa Akon. Nafurahi sana sasa video hii iko tayari baada ya mashabiki wangu kuisubiri kwa muda mrefu. Natumaini nyimbo yangu itafanya vizuri ndani na nje ya nchi na kunipa fursa ya kuwa mwanamuziki nyota na hii ndio imekuwa ndoto yangu. Nawaomba watanzania waniunge mkono ili nyimbo zangu na muziki wangu uendelee kufanya vizuri.”

Aliongeza kwa kusema ”Napenda pia kuchukua nafasi hii kuwapongeza washiriki wa mwaka huu walioingia tano bora na kuwashauri waweke juhudi na nia ili waweze kujinyakulia ushindi na hatimae kutuwakilisha vyema katika mashindano ya Afrika na kurudi na ushindi nyumbani”. Aliongeza Mayunga

Naye Meneja uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando alisema , tunajivunia kuendelea kuwawezesha watanzania kuonyesha vipaji vyao ndani na nje ya nchi kupitia shindano hili la Airtel Trace Music Stars . Tunaamini video ya Mayunga itafanya vizuri  ikiwa watanzania tutamuunga mkono Star wetu huyu,  nachukua fursa hii  kuwaomba wadau mbalimbali wa tasnia ya muziki  kuisikiliza na kuipiga katika vyombo mbalilmbali kama radio, TV na klabu za muziki ili iwafikie mashabiki wengi”

Kufatia ushindi wake Nalimi Mayunga ameweza kupata mafunzo ya muziki toka kwa Akon pamoja na kurekodi kibao hicho kipya cha “Please don’t go away” na pia amepata nafasi ya kurekodi upya wimbo wake nchini South Afrika ujulikanao kama “Nice Couple”ambao unaendelea kufanya vizuri sana kwa sasa
Share on Google Plus

About feisal pinto

Computer Application Student, Author, Short Stories Writer, Business Proposal Writer, Presenter and Application Builder. Email feisalpinto4@gmail.com for complains and business only.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

ad